Methali |
---|
Maamkizi |
Heshima na adabu |
Vitate |
Semi na nahau |
Tashbihi |
Istiara |
Shada/takriri |
Tanakali |
Ushairi |
Vitendawili |
Tashbihi jozi |
Maswali kadirifu |
- Shada ni maneno yanayotumika kutilia mkazo au kusisitiza hali fulani.
Mifano ya shada:
1. Furaha na buraha - furaha tele.
2. Maskini hohehahe - maskini kupita kiasi.
3. Simanzi na majonzi - huzuni kubwa.
4. Ugonjwa usiosikia dawa wala kafara - ugonjwa usiotibika.
5. Waganga na waganguzi - mabingwa wa tiba.
6. Zogo na zahama - fujo na ghasia nyingi.
7. Kujitahidi kufa kupona - kujitahidi sana.
8. Rafiki wa kufa kuzikana - rafiki mkuu.
9. Daima dawamu - bila kukoma; kila wakati.
10. Miaka nenda miaka rudi - miaka mingi.
11. Miaka na mikaka - miaka mingi.
12. Miaka na dahari - miaka mingi.
13. Balaa na belua - matatizo makubwa.
14. Kinagaubaga Dhahiri shahiri - waziwazi; bila kuficha.
15. Bure bilashi - bila sababu yoyote ile.
16. Salama salimini -bila hatari yoyote ile.
17. Nadra na adimu -uhaba mkubwa, si rahisi kupatikana.
18. Uvumba na ubani Udi na ambari -kwa bidii sana.
19. Kwa mapana na marefu -kwa kila njia.
20. Hapiki hapakui -mzembe mno.
21. Kutojali togo wala jando -kutojali kwa vyovyote vile.
22. Kuwaza na kuwazua -kufikiria sana.
23. Kutia na kutoa -kufikiria sana.
24. Ndugu wa toka nitoke -ndugu waliozaliwa na mama mmoja na wapendanao.
25. Si hayati si mamati -kuugua sana.
26. Hajijui hajitambui -kuchanganyikiwa k.m. kutokana na uuele, umaskini, ulevi n.k.
27. Hana kazi wala bazi -hana kazi yoyote ile.
28. Kutwa kucha -mchana na usiku, kila wakati
29. Hajailalia hajaiamkia -hajaitarajia, jambo ambalo. hulitarajii kamwe.
30. Asili na jadi -zamani sana.
31. Haliki hatafuniki -utundu uliopita kiasi.
32. Haambiliki hasemezeki
33. Hakanywi hakanyiki -Utukutu uliopita kiasi
34. Shangwe na hoihoi Vifijo na nderemo - furaha na kushangilia.
35. Raha mustarehe -bila taabu au usumbufu wowote.
36. Haoni hasikii -kupumbazwa au kulipenda. jambo kupita kiasi.
37. Ima fa ima -bila kujali.
38. Liwalo na liwe
39. Upende usipende - lazima.
40. Hali na mali - kwa kila hali.
41. Tunu na tamasha - kwa kila hali ya furaha.
42. Hayanihusu ndewe wala sikio
43. Hayanihusu damu wala usaha -hayanihusu kwa kila hali.
44. Hazidishi hapunguzi -hayana athari yoyote
45. Misitu na nyika -safari ndefu.
46. Mabonde na milima -safari ndefu.
47. Mito na maziwa -safari ndefu.
48. Kiguu na njia -kutembea sana.
49. Hana harusi hana matanga
50. Hana ngoma hana maulidi -kutokuwa na furaha.
51. Inda na inadi -kuwa na wivu na chuki.
52. Kuanzia shina hadi kilele -kila sehemu kila jambo.
53. Hana hanani Sina sinani -umaskini wa kupindukia.
54. Hana hatia wala taksiri - hana hatia yoyote.
55. Nipe nikupe -kuwa na masharti
56. Kwa heri na kwa shari -kwa uzuri na kwa ubaya.
57. Hakiri habali -hakubali jambo.
58. Juu chini -kwa bidii sana.
59. Kuduwaa na kubung’aa -kushtuka/kushangaa sana.
60. Hana bee wala tee -maskini kupindukia.
61. Matatizo na majojo -matatizo tipitipi.
62. Wahenga na wahenguzi -wazee wa zamani waliokuwa na hekima.
63. Kilele na kilelecha -sehemu ya juu kabisa ya kitu au hali.
64. Enzi na dahari -tangu zamani.
65. Kunawiri na kushamiri -kufanikiwa sana/kustawi sana.
66. Juha na majinuni -mjinga sana
67. Nia na azma -kusudi kuu.
Mifano katika sentensi
1. Ingawa alikuwa amekanywa kupita msituni hakujali togo wala jando. Alipita kuko huko.
2. Maskini shaibu huyo alipatwa na simanzi na majonzi alipoarifiwa mauti ya mwanawe.
3. Tuliandamana na rafiki yangu wa kufa na kuzikana hadi hospitalini.
4. Mzee huyo aliniadhibu bure bilashi bila hatia wala taksiri.
5. Timu hiyo ilitafuta bao la ushindi kwa udi na ubani lakini haikufua dafu.
6. Tulipatana na balaa na belua gari letu lilipoharibika katikati ya gongo la msitu.
7. Mgonjwa huyo hajui aingiaye wala atokaye. Yu katika pumzi zake za mwisho.
8. Alitaka kuniingiza katika ugomvi wao lakini uhusiano wao haunihusu ndewe wala sikio.
9. Kijana yule haliki hatafuniki. Ninakwambia hasikii la mwadhini wala la mteka maji msikitini.
10. Alinieleza masaibu yake kuanzia shina hadi kilele lakini nisingemsaidia kwani hata mimi sina sinani.