Methali |
---|
Maamkizi |
Heshima na adabu |
Vitate |
Semi na nahau |
Tashbihi |
Istiara |
Shada/takriri |
Tanakali |
Ushairi |
Vitendawili |
Tashbihi jozi |
Maswali kadirifu |
- Istiara hutumika kulinganishia hali.
- Hata hivyo, katika istiara, sifa inayolinganishwa haitajwi wala viunganishi mithili ya, ja, na kama havitumiki. Mifano:
1. Baba yake ni simba – mkali.
2. Jirani yangu ni shetani/ibilisi – katili, asiye na huruma.
3. Mwenzake ni mchwa – ana bidii.
4. Kakangu ni mbwakoko – mzururaji.
5. Mjakazi wetu ni chiriku – anaongea sana.
6. Kambi hiyo ni shimo la mateso – kuna mateso chungu nzima.
7. Nyumbani kwa msena wangu ni paradiso – ni kuzuri na kuna amani.
8. Mjombangu ni ndumakuwili – ni mnafiki.
9. Mwalimu wetu ni unju – ni mrefu sana.
10. Mwanamke huyo ni kasuku – anapenda kuyaiga mambo.
11. Chakula kile ni shubiri – ni kichungu mno.
12. Nguo ya kasisi ni theluji – ni nyeupe sana.
13. Mzigo wa wale ni nanga – ni mzito sana.
14. Yeye ni bahari – anaelewa mambo mengi.
15. Mgonjwa huyo ni mfupa – amekonda sana.
16. Upanga huo ni wembe – ni mkali sana.
17. Mwanariadha yule ni duma – ana mbio sana.
18. Nyumba ya halati wangu ni kasri – ni kubwa na ya kifahari.
19. Mwanasiasa yule ni kinyonga – ni kigeugeu.
20. Mpangaji yule ana ndimi mbili – ni kigeugeu.
21. Bintiye ni malaika – ni mrembo.
22. Kitoto chake ni fugo – ni kichafu.
23. Mamangu ni msamaria mwema – anapenda kusaidia na ni karimu.
24. Mwenzangu ni baniani – ni mnyimi.
25. Kakaye ni chui – anaonekana mpole lakini ni mtu hatari.
26. Mzee huyo ni panya – ni mnafiki.
27. Dadaye ni mbilikimo – ni mfupi sana.
28. Mimi ni tembo – nina nguvu nyingi za mwili.
29. Njaa ni adui mkubwa – njaa inaleta maafa.
30. Kinywa chake ni pango chafu – ana mazoea ya kutoa maneno ya kuudhi.
31. Mvulana huyo ni mpingo – ni mweusi sana.
32. Elimu ni nguzo maishani – Elimu ina umuhimu mkubwa maishani.
33. Mambo hayo ni usiku wa giza – hayaeleweki.
34. Maneno ya mwalimu huyo ni lulu – yanapendeza na yana busara.
35. Kinywaji alichotuandalia kilikuwa ni asali – kilikuwa kitamu sana.
36. Seremala yule ni sungura mjanja – ana ujanja wa kudanganya watu.
37. Moyo wake ni msitu mkubwa – ana siri nyingi moyoni mwake.
38. Mja huyu ni fisi – ni mlafi na mwenye tamaa.
39. Pesa ni mvunja mlima – zina uwezo mkubwa.
40. Mwimbaji huyu ni kinanda – anajua kuimba.
41. Maskini jirani huyu ni kupe – ni mzembe apendaye kutegemea jasho la wengine.
42. Pesa ni sabuni ya roho – pesa hufurahisha na huburudisha.
[resource: 3664, align: left]
43. Timu hiyo ni mwamba – haishindiki.
44. Maswali yale yalikuwa mboga – yalikuwa rahisi mno.
45. Maswali hayo ni mawe – ni magumu sana.
46. Mamaye ni bata – mpole na apendaye kudekeza.
47. Macho ya mwizi yule yalikuwa ni damu – yalikuwa mekundu mno.
48. Bintiye ni tausi – anaringa sana.
49. Gari lake ni dhahabu – ni ghali na la thamani ya juu.
50. Kinywaji alichompa kilikuwa ni barafu – kilikuwa ni baridi sana.