Semi na nahau
Nahau ni maneno yenye maana maalum ambayo hayajatokana na maana za kawaida za maneno hayo.
Zifuatazo ni nahau za kuelezea hali mbalimbali
- kuoa – kupata jiko, kuasi ukapera, kufunga ndoa/nikahi/nikaha, kufunga pingu za maisha.
- kufanya bidii – kujifunga nira, kujifunga masombo, kujifunga kibwebwe.
- kufa – kwenda jongomeo, kwenda kuzimuni, kufuata njia ya marahaba, kupungia dunia mkono wa buriani, kutangulia mbele ya haki, kuipa dunia kisogo, kukata kamba, koma moyo
- kuwa mzembe – kulaza damu, kuwa kupe, kuwa chaza, kuwa na mkono mzito.
- kupona – kupata nafuu, kuona ashekari, kuona afueni.
- kuwa na bahati – kuwa na ndege mzuri, kushukiwa na nyota ya jaha, kuwa na mkono mzuri
- kuvumilia matatizo – kuuma meno, kumeza mate machungu.
- kufukuzwa kazini – kupigwa kalamu, kuonyeshwa mlango, kuonyeshwa paa, kumwaga unga.
- kuharibika kwa jambo au mambo – mambo kwenda mrama, mambo kwenda shoto, mambo kwenda upogo, mambo kwenda segemnege, mambo kutumbukia nyongo.
- kupuuza – kutemea mate, kuonyesha mgongo, kuvalia miwani, kufumbia macho.
- kuongea maneno ya busara – kutoa lulu.
- kuongea maneno yasiyo na maana – kutoa ngebe, kutoa maneno ya mkahawani.
- kudanganya – kutia kiwi, kupaka mafuta kwa tako au kwa mgongo wa chupa, kumpatia mtu ulimi wa kulazia, kupiga mafamba, kuuza upepo kwa dunia,
- kucheza kayaya za chini kwa chini - kujuta – kuuma vidole
- kukimbia hatari – kuchana mbuga, kutimua mbio, kutoka shoti, kusema mguu niponye, kuponda wa fisi, kutwika miguu mabegani.
- kutembea – kupiga miguu, kupiga milundi.
- kulewa pombe – kupiga maji, kuvaa miwani, kuchapa mtindi.
- kukasirika – kupandwa na mori, kupandwa na mafutu, kuchemkwa na damu, kuchemkwa na nyongo, kupandwa na madadi.
- kufikiria sana – kujikuna kichwa.
- kupatwa na matatizo – kupigwa na urumo, kula mumbi, kuogelea kwenye mchanga wa moto, kuingia kwenye maji makuu, maji kuwa ya shingoni, kuingia kwenye tanuri la moto, maji kuzidi unga.
- kuwa na tamaa – kuwa na mate ya fisi, kumezea kitu mate
- kuomba kwa Mola – kupiga dua, kupiga bisimillahi
- kuwa na njaa – kubanwa na kapu.
- kula chakula – kushtaki njaa, kufanyia mlo/chakula haki.
- kukamatwa – kutiwa mbaroni, kutiwa nguvuni.
- kufungwa gerezani – kula kalenda.
- kuzungumza – kupiga soga, kula gumzo, kula nyama ya ulimi.
- kupoteza matumaini – kufa moyo, kuvunjika moyo, kukata tamaa.
- kupotea njia – kukanyaga chechele
- kutoa rushwa – kuzunguka mbuyu, kupiga konde la nyuma, kutoa mlungula.
- kupata upinzani – kutolewa jasho,
- kutolewa kamasi - kukonda, kuwa fremu, kuwa gofu,
- kukaukwa na damu, - kuwa mfupa.
- kumkanya mtu – kumshika sikio.
- kumpa mtu pole – kumpa mkono wa tanzia.
- kuwa mchoyo – kuwa na mkono wa birika/buli, kuwa joka la mdimu.
- kuongoza – kushika usukani, kushika hatamu za uongozi.
- kuondoka – kung’oa nanga.
- kuwa wa mwisho – kushika mkia, kushika nanga.
- kufikia mwisho – kutia nanga, kufikia ukingoni.
- kufitini – kutia fitina, kutia chuku, kutia utambi, kuchoma nguru.
- kumaliza kiu ya maji – kukata kiu, kukonga roho.
- kumwomba mtu msamaha – kumwangukia mguuni.
- kumheshimu mtu – kumvulia kofia, kumshika miguu.
- kufanya kazi – kuzimbua riziki, kutafuta unga, kushika mpini, kumwaga jasho.
- kumwaibisha mtu -kumvunjia mtu mbeleko, kumvua mtu nguo. kumpaka mtu mavi, kumpaka mtu vumbi.
- kumtia kiraka - kuwa adui, kutopaliana moto, kutopikika katika chungu kimoja, kuwa maji na mafuta.