- Ngeli hii inajumuisha nomino za vitu visivyo na uhai. Ngeli hii ina makundi matano ya nomino.
i. Nomino ambazo umoja huanza kwa u na wingi tunaondoa u k.m. unywele, ukuta, ufagio, ufunguo, unyasi, utepe, utosi, ukoo, upote, upenu, upondo, upongoo, upanga, upepeo n.k.
ii. Nomino ambazo umoja huanza kwa u wingi zinaanza kwa ny k.m. uta, ufa, uwanja, uso, uwayo, uzi, uwalio, ugwe.
iii. Nomino ambazo umoja huanza kwa w na wingi huanza kwa ny k.m. waraka, wakati, wembe, wimbo, wayo, waya, wavu, wanja, wanda, wadhifa, waadhi.
iv. Nomino ambazo umoja huanza kwa u na wingi huanza kwa nd k.m ulimi, uele.
v. Nomino ambazo umoja huanza kwa u na wingi huanza kwa mb k.m ubao – mbao, ubavu – mbavu, ubati – mbati, ubale-mbale
Umoja: Ukuta unaokarabatiwa ni mrefu.
Wingi: Kuta zinazokarabatiwa ni ndefu.
Umoja: Ufunguo huo ndio wangu.
Wingi: Funguo hizo ndizo zetu.
Umoja: Ufunguo huo sio wangu.
Wingi: Funguo hizo sizo zetu.
Umoja: Utepe huu nao ni imara.
Wingi: Tepe hizi nazo ni imara.
Umoja: huu huo ule.
Wingi: hizi hizo zile.
Umoja: uu huu uo huo ule ule.
Wingi: zizi hizi zizo hizo zile zile.
Umoja: huu huu huo huo ule ule Wingi: hizi hizi hizo hizo zile zile.
Umoja: Uzi wenye fundo haushonei vizuri.
Wingi: Nyuzi z e n y e mafundo hazishonei vizuri.
Umoja: Ubao wenyewe unapendeza.
Wingi: Mbao zenyewe zinapendeza.
Umoja: Waya wote umetumika.
Wingi: Nyaya zote zimetumika.
Umoja: Nitautumia wavu wowote kuvulia.
Wingi: Tutazitumia nyavu zozote kuvulia.
Umoja: Ameupokea waadhi mwingine.
Wingi: Wamezipokea nyaadhi nyingine
Wingi: Jirani amepokea nyaraka nyingi.
Umoja: Umesoma silabi za ukwapi upi?
Wingi: Mmesoma silabi za kwapi zipi?
Wingi: Je, ng’ombe ana kwato ngapi?
Mmoja, mbili, tatu, nne, tano, sita, saba, nane, tisa, kumi, kumi na mmoja, kumi na mbili, kumi na tatu, kumi na nne, kumi na tano