Ngeli ya LI - YA
Ngeli ya LI-YA
Ngeli hii huwa na aina tatu za nomino
- . Nomino zote katika hali ya ukubwa k.m. jitu, toto, jia, buzi, gombe, lango, jumba, jito n.k.
- Nomino za vitu ambazo katika hali ya umoja huchukua viambishi mbalimbali lakini wingi huchukua kiambishi ma- k.m gari -magari, swali -maswali, jicho -macho, vumbi – mavumbi
- Nomino za vitu ambazo katika hali ya umoja huchukua viambishi mbalimbali lakini wingi huchukua kiambishi m e k.m. jino – meno
- Vivumishi Kiwakilishi amba- Umoja: Tunda ambalo anakula halijaiva. Wingi: Matunda ambayo wanakula hayajaiva.
- 'O' rejeshi Umoja: Tunda analokula halijaiva. Wingi: Matunda wanayokula hayajaiva.
- Ndi- ya kusisitiza Umoja: Jizi hili ndilo lililonishambulia. Wingi: Majizi haya ndiyo yaliyotushambulia.
- Si- ya kukataa Umoja: Jizi hili silo lililotoroka. Wingi: Majizi haya siyo yaliyotoroka.
- Na- ya kirejelei Umoja: Jino hili nalo limeniuma kwa siku nyingi. Wingi: Meno haya nayo yametuuma kwa siku nyingi.
- Viashiria/vionyeshi Umoja: hili hilo lile Wingi: haya hayo yale.
- Viashiria/vionyeshi visisitizi Umoja: lili hili lilo hilo lile lile Wingi: yaya haya yayo hayo yale yale.
- Viashiria/vionyeshi radidi Umoja: hili hili hilo hilo lile lile Wingi: haya haya hayo hayo yale yale.
- Kivumishi -enye Umoja: Gari lenye hitilafu ya mtambo ni hatari kusafiria. Wingi: Magari yenye hitilafu za mitambo ni hatari kusafiria.
- Kivumishi -enyewe Umoja: Tawi limevunjika lenyewe. Wingi: Matawi yamevunjika yenyewe.
- Kivumishi -ote Hutumika kuonyeshea ukamilifu wa kila sehemu k.m Darasa lote limefurika. Umoja: Darasa lote limepambika. Wingi: Madarasa yote yamepambika.
- Kivumishi -o-ote Umoja: Mpishi atalitumia jiko lolote litakalopatikana. Wingi: Wapishi watayatumia majiko yoyote yatakayopatikana.
- Kivumishi -ngi Umoja: Uwanjani hakuna vumbi jingi. Wingi: Uwanjani hakuna mavumbi mengi.
Muhimu Kivumishi jingi hutumika kwa nomino chache tu katika ngeli hii ya LI-YA. k.m vumbi, tunda, gari n.k.
- Kivumishi -ngine Umoja: Nitalijibu swali jingine iwapo nitaulizwa. Wingi:
- Tutayajibu maswali mengine iwapo tutaulizwa. Kiulizi -pi? Umoja: Baba alilitumia gari lipi? Wingi: Akina baba waliyatumia magari yapi?
Kiulizi -ngapi Wingi: Wasafiri waliyatumia magari mangapi?