Matumizi ya kina na akina
Maneno haya hutumika kuelezea watu wa hali moja k.v. tabia, kiwango (utajiri au umaskini) au ukoo mmoja. Kwa kawaida, maneno haya huonyeshea wingi au kundi. Iangalie mifano ifuatayo
1. Wasalimie kina nyanya na babu, aidha kina shangazi na mjomba.
2. Tulienda kuwajulia hali kina Musa na Fatuma.
3. Akina Juma walialikwa shereheni.
4. Akina mama walihudhuria kongamano hilo.
5. Akina shemeji wanapenda chapatti kwa mchuzi wa kuku.
Kwa kawaida akina hutumiwa tunapoongea kuhusu kundi moja la watu wenye tabia au hali sawa k.m. akina dada – dada wengi, akina mama – mama wengi.
Kina nayo hutumika tunapoongea kuhusu zaidi ya kundi moja la watu k.m. kina dada na kaka, kina mama na baba.