- Hivi ni vihusushi vya mahali.
- Huonyesha uhusika au kuwapo kwa kitu kilichotajwa mahali fulani.
- Ukiambatanisha jina lolote na -ni basi jina hilo hubadilika na kuwa 'mahali pa' au mahali ku' au 'mahali mu'.
Mifano
kikapi - kikapuni
mti - mtini
gari - garini
nyumbani - nyumbani
uwanja - uwanjani
Silabi ni ina matumizi mbalimbali. -ni ya wingi.
Ni ikiwekwa mwishoni mwa kitenzi au kiarifu huashiria wingi. k.m. Njoo hapa (umoja) – Njooni hapa (wingi) Simama hapa (umoja) – Simameni hapa (wingi) -ni ya mahali (ni ya kihusishi)
Ni ikiwekwa mwishoni mwa nomino ya kitu, nomino hiyo hubadilika na kuwa nomino ya mahali. Nyumba (kitu) - Nyumbani (mahali) Nimefika katika soko - Nimefika sokoni.
Tahadhari -ni ya mahali itumikapo, vihusishi vifuatavyo havitumiki: ndani ya, katika, kwenye Ni- ya nafsi Ni-huashiria nafsi ya kwanza umoja. k.m. (mimi) Ninajitahidi.
Ni ya kiunganishi Huashiria:
Wakati huo huo kiambishitamati - ni kina maana sawa na 'katika', 'kwenye' na 'ndani ya'. Kwa hivyo vihusishi hivi havitumiki kamwe wakati mmoja kwenye sentensi moja.
Mifano:
1
i) Vitabu vimo kwenye gari.
ii) Vitabu vimo katika gari.
iii) Vitabu vimo ndani ya gari.
iv) Vitabu vimo garini.
2
i) Mhazili ametoka katika ofisi.
ii) Mhazili ametoka ndani ya ofisi.
iii) Mhazili ametoka kwenye ofisi.
iv) Mhazili ametoka ofisini.
Kiambishitamati - ni kikiongezwa mwishoni mwa nomino,mana inayopatikana ni ile ya mahali.
Mifano:
shule - shuleni
barabara - barabarani
nyumbani - nyumbani
Mifano ya sentensi:
Mama anauza mboga sokoni.
Dada haondoki nyumbani.
Mwalimu yuko darasani.
Kutumia kihusishi cha kwa ukiwa na maana ya ni,katika,kwenye au ndani ya ni kosa. Kwa hiyo:
USISEME: Vitabu vimo kwa sanduku. WALA: Kaka yuko kwa chumbani.
Kwa ni kihusishi cha mahali kinachotumika tu tunapotaja uhusiano kati ya mahali na MTU au WATU. Tazama:
TUNASEMA: Nimetoka kwa daktari.
AU: Tunaishi kwa wazazi
AU: Alitoka kwa shangazi
- Baada ya kuambatanisha nomino yoyote na - ni, viambishi vyote hubadilika na kuwa vya MAHALI. Tazama jedwali hili kwa kudadisi mabaliko ya viambishi katika vivumishi hivi:
Tumia kidokezi ulichopewa mabanoni kusanifisha sentensi hizi.
Mfano:
Kijiji chao kina usalama.( tumia:PA)
Kijijini pao pana usalama.
1. Shamba lililolimwa ni zuri. ( tumia: KU)
2. Mto huu mkubwa hauvukiki. ( tumia: PA)
3. Chumba chake ndicho kilichopambwa. (tumia: M)
4. Mlima wenyewe hauna theluji. ( tumia:KU)
5. Katika kabati lile mna vikombe. ( tunia : M)
Kosoa sentensi hizi.
1. Helena aliingia darasa akakaa kwa dawati lake.
2. Musa alitoka nyumba akaingia garini la rafikiye.
3. Mwalimu alitoka kwa ofisi akaingia kwa darasa la wanafunzi.
4. Jara na roda wanakaa kitini kimoja darasa letu.
5. Katika shuleni yetu ina miti mingi sana.