Viulizi
Viulizi hutumika kuulizia mahali, wakati, mtendaji n.k.
Tunavyo viulizi kama vile.
Huulizia wakati au muda k.m. Ulifika lini shuleni?
Huulizia mtendaji au kitendaji k.m. Ni chombo gani kimezama?
Muhimu
Kiulizi gani hakichukui kiambishi chochote.
Hutumika sawa na gani? Hata hivyo, kiulizi –pi? huchukua viambishi mbalimbali kulingana na ngeli. K.m. Anatumia kalamu
Anatumia kisu kipi?
Anatumia gari lipi?
Hutumika katika sehemu mbili:
1. Kuulizia hali /jinsi/ namna ya jambo k.m Ulifika vipi?
2. Hutumika kwa kiulizi –pi? katika ngeli ya KI-VI hali ya wingi k.m. Tutatumia vitabu vipi?
Hutumika kwa njia mbili.
1. Kuulizia mahali k.m. Anaishi wapi?
2. Katika ngeli ya A-WA (wingi) katika kiulizi –pi? k.m. Ni watu wapi waliofika?[resource: 3422, align: left]
Huulizia idadi. Hutumika tu katika hali ya
wingi. k.m. Ni vitoto vingapivimefika?
K i u l i z i – n g a p i h u c h u k u a v i a m b i s h i
mbalimbali kulingana na ngeli?
(Iangalie sehemu ya kwanza –Ngeli)
Huulizia mtendaji k.m. Ni nani anayemlisha mtoto?
Ni akina nani waliowatumbuiza wageni?
Muhimu
Kiulizi nani ?hutumika katika ngeli ya (A-WA) pekee.
Hutumika kuulizia kitu au tendo linalotendwa
k.m. Unafanya nini?
Hutumika kuulizia sababu ya jambo k.m.
Kwa nini umechelewa kufika shuleni?
Kiswahili golden tips sarufi.2b 8/2/12 3:51 PM Page 44 45
Hutumika kuulizia hali k.m. Mtoto alianguka aje?
Viulizi: - ngapi na - pi ni viulizi vinavyochukua viambishingeli mbalimbali.
Tazama jedwali lifuatalo:
Tumia kiulizi sahihi kisarufi ukamilishe sentensi zifuatazo.
1. Kucheza _____ (kugani, ipi, upi,kupi) kunakokufurahisha?
2. Maskani _____ (mapi, magani,yapi,ipi) yenye hewa safi?
3. Maiti _____ ( ipi, yapi, yupi,zipi) huzikwa bila sanda?
4. Vitabu vimo mkobani _____ ? ( upi, mpi, ipi, nini)
5. Baba alimtuma _____? ( gani,wepi, nani,upi)
6. Mtachezea uwanjani _____? (upi,ipi, papi,ngapi)
7. Huku ni kwa watu _____ ? ( ngapi, yupi, gani,kupi)
8. Ulitumia jina _____ ? ( jipi, ipi,lipi,ngapi)
9. Nyumba yenu itajengwa _____? (gani, ngapi, ipi, vipi)
10. Mitume _____ ( ngapi,mingapi,wangapi,mangapi) hujulikana duniani?