- Vihisishi huonyeshea hisia za ndani. k.m.
• Hisia za mshangao.
• Hisia za huzuni.
• Hisia za furaha.
• Hisia za majuto.
• Hisia za huruma au masikitiko.
Tutumiapo vihisishi kihisi (!) hutumika.
1. Lo! - hutumika kuonyesha mshangao, furaha, hofu au mshtuko na hali ya kubung'aa.
2. Masalale! - huonyesha mshangao
3. Do! au Du! - huonyesha mshangao; hali ya kutoamini.
4. Salaala! - huonyesha mshangao wa hali ya juu.
5. Ebo! - huonyesha mshangao; hali ya dharau na kutoamini.
6. Aka! - huonyesha mshangoa; hali ya kukanusha jambo.
7. Ah! - huonyesha hali ya kukereka.
8. Ahaa! - huonyesha furaha; uchungu;kukubali;kukataa.
9. Aa! - huitikia; kukubali; kukataa; hali ya kuchanganyikiwa.
10. Po! - huonyesha dharau.
11. Pukachaka! - huonyesha kukidharau kitu; kutokithamini kabisa.
12. Oyee! - huonyesha furaha, shangwe na hali ya kupongeza.
13. Yarabi masikini! - hushangaa na kuomba msaadakwa mwenyezi Mungu.
14. Ewaa! - huonyesha kuitisha kuwa mambo ni sawa.
15. Hewaa! - hukubali kuwa mambo ni sawasawa;barabara!
16. Taib! - hukubali kuwa ni vyema au vizuri.
17. Shabash! - huonyesha furaha au mshangao wa hali ya kuridhishwa.
18. Ala! - huonyesha mshangao au mshtuko.
19. Aisee! - humfanya mtu asikilize unayotaka kumwambia; ohaa! abaa!
20. Cho! - huonyesha mshangao; lo! cha!
21. Chup! - humwambia mtu anyamaze kwa hasiraau dharau; kimya! chub!
22. Us! - humnyamazisha mtu kwa hasira au dharau.
23. Ehee! - huonyesha ukubaliano au hamu ya kuendelea kusikiliza; ehee!
24. Epuu! - huonyesha kutompa mtu hima ya kufanya au kutamka alilonuia; kutoamini analotamka.
25. Ewe! - huonyesha mshangao na mgutuko.
26. He! - huashiria wito wa kuhadharisha.
27. Aa-aa! - hunyamazisha, huzomea au kukemea.
28. Oh! - huonyesha mshangao; kutoamini yaliyosemwa.
29. Oofuu! - huonyesha uchovu au kuvuta pumzi kwa uchovu.
30. Mmh! - hali ya kutoamini unaloambiwa.
31. Afanalek! - huonyesha kupigwa na butwaa, kushtuka.
32. Audhubillahi! - huonyesha mshangao na kumlaani shetani.
33. Mnh! huashiria kuitikia kwa wasiwasi, hofu na mshangao.
34. Hee! - huonyesha mshtuko wa kutahadharisha au kuonya.
35. Ohoo! - hukashifu.
36. Zii! - hukemea; hulaani; kinyume cha kushangilia.
37. Yarabi Stara! - huashiria kuomba ulinza na Mwenyezi Mungu.
1. kukereka
2. kupongeza
3. kuhimiza
5. kunyamazisha