Vimilikishi ni maneno yanayoonyesha hali ya kuwa na kitu, yaani kumiliki (ya kutamalaki). Kwa kawaida katika lugha ya Kiswahili, vimilikishi hutegemea hali mbili: nafsi na ngeli ya nomino husika. Ili kuelewa vimilikishi sharti mwanafunzi aelewe kwa kina nafsi zote tatu na pia ngeli zote za Kiswahili. Vimilikishi vya nafsi moja vitabadilika kulingana.
Soma mifano ifuatayo:
Nafsi ni ile ile lakini nomino ni katika ngeli mbalimbali ndiposa vimiliki vimebadilika. Vilevile vimiliki vitabadilika kulingana na nafsi ya mmiliki mhusika.
Tazama sentensi zifuatazo:
Muhimu
Katika hali ya umoja:
Basi, iwapo unatakikana kuandika wingi wa vimiliki sharti ukumbuke kuzungumzia nomino zote mbili katika hali ya wingi.
Tazama jedwali lifuatalo kwa makini
Nafsi
Ngeli Nomino kwanza pili tatu
(sisi) (nyinyi) (wao)
A-W A watoto wetu wenu wao
KI-VI vyungu vyetu vyenu vyao
LI-Y A mashati yetu yenu yao
U-I mitego yetu yenu yao
U-ZI fito zetu zenu zao
I-ZI nguo zetu zenu zao
U-YA matete yetu yenu yao
I-I damu yetu yenu yao
YA-YA mate yetu yenu yao
U-U ukakamavu wetu wenu wao
PA-PA darasani petu penu pao
KU-KU dukani kwetu kwenu kwao
M-M pambajioni mwetu mwenu mwao
Je, umegundua lolote kuhusiana na silabi za
mwisho za vimilikishi?
Hivi ni vimilikishi vinavyokatwa na kisha
k u u n g a n i s h w a n a j i n a l a j a m a a . K w akawaida, ili tuwe na vimilikishimikato au
vimilikishiambata, lazima tuwe na nomino na
kimiliki.
Vimilikishimikato hutumika katika majina
ya nasaba pekee.
Kuna njia mbili za kupata vimili-kishimikato:
kimilikishi na kuiunganisha na nomino
miliki k.m mama yangu – mamangu,
mwana wangu – mwanangu, mjomba
wake– mjombake
mwisho ya kimilikishi na kuiunganisha
na nomino miliki k.m mjomba wake–
mjombawe, mama yako – mamayo
Tahadhari:
Vimilikishi vyenye irabu tatu havitumiki
katika vimilikishimikato k.m. mjomba wao,
mama yao