Kwa lugha rahisi na ya moja kwa moja tunaweza kusema nafsi ni sawa na “mtu”. Katika lugha ya Kiswahili tunazo nafsi tatu:
Nafsi ya kwanza Mimi – huwakilishwa na ni.
Sisi – huwakilishwa na tu.
Nafsi ya pili Wewe – huwakilishwa na u.
Nyinyi – huwakilishwa na m.
Nafsi ya tatu Yeye – huwakilishwa na a.
Wao – huwakilishwa na wa.
Viwakilishi
Kiwakilishi ni neno au silabi inayosimama badala ya nomino au kitenzi. Viwakilishi vya nafsi ni kama vifuatavyo.
Nafsi Kiwakilishi Matumizi
Nafsi ya kwanza |
Mimi |
Nitasoma kwa bidii |
Sisi |
Tutasoma kwa bidii |
|
Nafsi ya pili |
Wewe |
Utasoma kwa bidii |
Nyinyi |
Mtasoma kwa bidii |
|
Nafsi ya tatu |
Yeye |
Atasoma kwa bidii |
Wao |
Watasoma kwa bidii
|
Iwapo kitenzi kitanyambuliwa kiwe katika hali ya kufanyia, kiwakilishi cha wewe hubadilika kutoka u na kuwa ku. k.m
Utaandika barua (kufanya) - Nitakuandikia barua (kufanyia).
Yeye nacho huwa m badala ya a k.m. Alimcheka (kufanya) - Nilimcheka (kufanyia)
Viashiria vinaweza kutumika kama viwakilishi. Kiashiria huwa kiwakilishi kinapotumika badala ya nomino au kitenzi kinachoashiriwa. Kwa hivyo, hakitaandamana na nomino au kitenzi husika.
Ziangalie sentensi zifuatazo: Mtu huyu ana bidii - kiashiria Mtu huyu ana bidii, yule ni mzembe. Huyu – kiashiria Yule – kiwakilishi – kinawakilisha mtu wa pili (ambaye ni mzembe).