Nomino za Kiswahili huwa katika hali tatu: wastani, udogo na ukubwa
Hali ya wastani Hali ya wastani ni hali ya kawaida. Wengine husema hali ya katikati. Katika hali hii, nomino huwa katikati. Si kubwa wala si ndogo. Aghalabu, nomino nyingi hutumiwa katika hali hii. Kwa mfano mtu, njia, ng’ombe, gari, mtoto, mti, kikapu n.k. Nomino katika hali ya wastani huwa katika ngeli mbalimbali kulingana na uwiano wa kisarufi.
Hali ya udogo Nomino huwa katika hali ya udogo inapodunishwa. Kudunishwa ni kufanywa iwe duni au ndogo k.m. mtu -kijitu, njia •kijia, ng’ombe - kigombe, gari - kigari, mtoto -kitoto, mti - kijiti, kikapu - kijikapu.
Nomino inapodunishwa, mabadiliko fulani hutokea
a) Nomino ambazo katika hali ya wastani zilikuwa na silabi mbili k.m. mtu – kijitu, mto – kijito
b) Nomino ambazo katika hali ya wastani zilikuwa katika ngeli ya KI - VI. Nomino hizi huongezewa silabi ji bila kuzingatia idadi ya silabi. k.m. kikapu – kij ikapu, kikombe – kijikombe
c) Nomino ambazo hupatikana katika ngeli ya LI-YA katika hali ya kawaida k.m. darasa – kijidarasa, tunda - kijitunda
Hali ya ukubwa Nomino huwa katika hali ya ukubwa inapofanywa kuwa kubwa k.m mtu - jitu, njia -jia, ng’ombe - gombe, gari - jigari, mtoto - toto, mti - jiti, kikapu - kapu/jikapu. Nomino zote katika hali ya ukubwa huwa katika ngeli ya LI-YA.
Nomino inapofanywa kubwa na kuchukua hali ya ukubwa, mabadiliko fulani hutokea.
Udogo Wastani Ukubwa kidomo mdomo domo kijikiti kiti jikiti kijijicho jicho jijicho kijijiko kijiko jijiko kijisichana msichana jisichana kikuta ukuta kuta kilango mlango lango kijibuyu kibuyu jibuyu kibuzi mbuzi buzi kijisu kisu jisu.
Udogo Wastani Ukubwa
Kidomo mdomo domo
Kijikiti kiti jikiti
Kijijicho jicho jijicho
Kijijiko jiko jijiko
Kijischana msichana jischana
Kikuta ukuta kuta
Kilango mlango lango
Kijibuyu kibuyu jibuyu
Kibuzi mbuzi buzi
Kijisu kisu jisu