- Ngeli ya PA huonyesha mahali HAPA, HAPO, PALE, ambapo ni mahali dhahiri, au wazi panapoeleweka au ambapo tuna habari kupahusu hata kama penyewe ni mbali.
- Viarifu vya ngeli hii huanza kwa pa- k.m Darasani panapambwa kwa matayarisho.
N/B Jina lolote linaweza kupachikwa kiambishi tamati -ni, nalo likawa au likageuka kuwa mahali HAPA, HAPO, PALE.
Mifano:
a) Nyumbani hapa pana vyakula vingi.
b) Nyumbani hapo pana vyakula vingi.
c) Nyumbani pale pana vyakula vingi.
Viwakilishi amba-
Sakafuni ambapo anafagia panateleza.
1. 'O' rejeshi
Sakafuni anapofagia panateleza.
2. 'Ndi' ya kusisitiza
Hamamuni anapooga ndipo hapa.
3. 'Si-' ya kukataa
Hamamuni anapo ogea sipo hapa.
4. 'Na-' ya kirejelei
Hapa napo pana watoto wengi.
5. Viashiria/vionyeshi: hapa, hapo, pale.
hapa hapa, hapo hapo, pale pale.
papa hapa, papo hapo, pale pale.
6. Kivumishi -enye
Sokoni penye wateja pana kelele.
7. Kivumishi -enyewe
Tuliogelea mtoni penyewe.
8. Kivumishi -ote
Mezani pote pana vitabu.
9. Kivumishi -o-ote
Nitakaa popote nitakapoonyeshwa.
10. Kivumishi -ngi
Hotelini pengi pana starehe.
11. Kivumishi -ngine
Alienda hotelini pengine palipompendeza
12. Kiulizi -pi?
Mjomba alienda shuleni papi?
Nyumbani pale pananipengeza - Nyumbani pale panatupendeza.
Shuleni palipofyekwa ni pangu. - Shuleni palopofyekwa ni petu.
3. Kiunganifu -A (pa)
Kitandani pa mtoto panafaa. - Vitandani pa watoto panafaa.
Chumbani penyewe pana baridi. - Vyumbani penyewe pana baridi.
Ubongoni penye nia pana njia. - Ubongoni penye nia pana njia.
Dukani pote pana bidhaa. - Madukani pote pana bidhaa.
Uwanjani popote mtu hununua bidhaa. - Nyanjani popote panafaa.
Tunduni pembamba pana mende mdogo. - Matunduni pembamba pana mende wadogo.
Ukutani pengine pana rangi. - Kutani pengine pana rangi.
Ukutani kwingi kuna rangi. - Kutani kwingi kuna rangi.
Jikoni pazuri pakubwa pana mlo. - Majikoni pazuri pakubwa pana mlo.
Uwanjani hapo hapana unyasi mrefu. - Nyanjani hapo hapana nyasi ndefu.
ZOEZI
Tia sentensi zifuatazo katika ngeli ya mahali (PA) kulingana na kiambishingeli ulichopewa mabanoni.
Mfano: Nyumba yangu ni nzuri = Nyumbani pangu ni pazuri.
1. Mlango ule una bawabu mkali.
2. Mlima wote umetanda ukungu.
3. Mto ule mkubwa una ngwena wakubwa.
4. Katika kisima kile mna maji safi.
5. Dika nilipendalo lina bidhaa marighawa.
6. Msitu wote ule waliuoalilia jana.
7. Anayelilima shamba hili hajalimaliza.
8. Gari lile jeupe limeibeba mizigo mingi.
9. Kitanda chako kizuri ndicho nitakachokilalia.
10. Maskani yoyote yakufaayo uyakimbilie, usisite.