Ngeli hii hujumuisha nomino za vitu visivyo na uhai.
Nomino za ngeli hii: • hubakia hivyo katika umoja na wingi, • hazihesabiki, na • huanza kwa silabi ma.
maji, mate, marashi, mafuta, madaraka, mamlaka, maisha, masuo, masira, maringo, maafa n.k.
Vivumishi vya ngeli hii ni sawa na vile vya ngeli ya LI-YA (hali ya wingi) Muhimu Ngeli ya YA-YA, haina vivumishi visifa vya idadi wala kiulizi –ngapi?
1. Viambishingeli ya - ya
i) Mazingira yangu yatunzwe. - Mazingira yetu yatunzwe.
ii) Maisha yako yanapendeza. - Maisha yenu yanapendeza.
2. Kirejeshi-O- (yo-yo)
i) Maji yasiyotunzwa usiyanywe. - Maji yasiyotunzwa msiyanywe
ii) Mate ambayo yamo kinywani ni machungu. - Mate ambayo yamo vinywani ni machungu.
3. Kiunganifu -A (ya-ya)
i) Maliwato ya nyumba hii ni safi. - Maliwato ya nyumba hizi ni safi.
ii) Mafuta ya kumpaka mtoto yameisha. - Mafuta ya kuwapaka watoto yameisha.
4. Vivumishi -enye na enyewe (ye- ye)
i) Maskani yenye chakula chema. - Maskani Yenye vyakula vyema.
ii) Mazingira yenyewe ni yenye mti mzuri. - Mazingira yenyewe ni yenye miti mizuri.
5. Vizumishi -enye na -o-ote (yo -yo)
i) Majira yote ya masika yana mvua ya kutisha. - Majira yote ya masika yana mvua ya kutisha
ii) Madhara yoyote yanatisha. - Madhara yoyote yanatisha.
6. Sifa -eupe, -eusi n.k. (me -me)
i) Mafuta meusi si ya mtoto huyu. - Mafuta meusi si ya watoto hawa.
ii) Maziwa si meusi ni meupe. - Maziwa si meusi ni meupe.
7. Sifa -ingi na -ingine (me-me)
i) Marashi mengi yanauzwa ghali dukani. - Marashi mengi yanauzwa ghali madukani.
ii) Mate mengine ni machungu kinywani. - Mate mengine ni machungu vinywani.
8) Vivumishi -zuri, -refu n.k (ma-ma)
i) Maziwa matamu ni mazuri kwangu. - Maziwa matamu ni mazuri kwetu.
ii) Maisha marefu ni bora kwa mtu kuliko mafupi. - Maisha marefu ni bora kwa watu kuliko mafupi.
9) Vikanushi (haya - haya)
i) Maji haya kunimwagikia. - Maji haya kutumwagikia.
ii) Majivuno hayana faida yoyote. - Majivuno hayana faida faida zozote.