Nomino
Nomino
- Nomino ni neno linalotaja jina la mahali, kiumbe, kitu, au hali. Pia huitwa jina au nauni. k.m. sokoni, kikombe, punda, werevu n.k.
- Uundaji wa nomino kutokana na vitenzi. Mtu atendapo kitendo, bila shaka kunakuwa na matokeo. Matokeo hayo huwa ni nomino k.m. Nikikimbia (kitenzi) matokeo huwa ni mbio (nomino).
Nomino kutokana na sifa Sifa ni neno ambalo huelezea mengi kuhusiana na nomino. Sifa hiyo inaweza kutoa nomino ambayo ni jina linalotaja sifa yenyewe k.m kubwa – ukubwa.
Tazama mifano ifuatayo:
- Sifa Nomino kutokana na sifa
refu urefu -geni ugeni -zuri uzuri -baya ubaya -gumu ugumu -chungu uchungu -ema wema -eupe weupe -nene unene -pya upya
Sifa zinaweza kuundwa kutokana na vitenzi. k.m Mtoto mtiifu hutii wakubwa wake. sifa kitenzi Mgeni mnyamavu alinyamaza sana. sifa kitenzi
Tazama mifano ifuatayo:
- Kitenzi Sifa soma msomaji ogopa mwoga iba mwizi chora mchoraji asi mwasi pika mpishi linda mlinzi suka msusi chokoza mchokozi jenga mjenzi