Kuna kanuni zinazofuatwa ili kubadilisha nomino kuwa katika hali ya ukubwa. Kwa mfano:
a) Jamii ya nomino zenye kianzo ki katika hali ya kawaida, huweza kugeuzwa katika ukubwa kwa kudondosha ki na kupachika ji.
Mifano:
kichwa - jichwa
kisima - jisima
kivuli - jivuli
b) Aina fulani ya nomino zinazoundwa au zinazotokana na silabi mbili, huweza kukubakika kudondosha silabi awali na kuambatisha ji kupata ukubwa.
Mifano:
mti - jiti
mwana - jana
mwehu - jehu
mfu - jifu
c) Kundi la nomino zinazoanza kwa ji hupachikwa ji tena ili kuunda ukubwa:
Mifano:
jina - jijina
jipu - jijipu
jitimai - jijitimai
jifya - jijifya
d) Nomino zozote zisizokuwa na mpangilio maalum wa vianzio vya viambishi jina huweza kupachikwa ji mwanzoni ili kupata ukubwa.
Mifano:
taa - jitaa
sahani - jisahani
redio - jiredio
shwa katika halimeza - jimeza
e) Nomino nyingine zinaweza kubadilishwa katika hali ya ukubwa baada ya kudondosha herufi ya mwanzo ya kianziojina. Aghalabu herufi zinazodondoshwa ni m au u endapo nomino hizo zinaanzia kwa: mb-, nd-, nj-, ng-
Mifano:
ngazi - gazi
ngamia - gamia
mbuga - buga
mbalamwezi - balamwezi
f) Jinsi nyingine ya kupata ukubwa ni kudondosha herufi ya mwanzo m katika nomino zozote zenye miundo au maumbo ya silabi tatu au zaidi zinazoanza kwa herufi m.
mlolongo - lolongo
mfereji - fereji
msumeno - sumeno
mguu - guu
Kumbuka majina yote ya ukubwa huorodhesha katika ngeli ya LI- YA. Kwa hivyo basi, jina lolote la ukubwa wingi wake huanza kwa silabi ma.
Mifano:
jijipu - majijipu
jitu - majitu
Domo - madomo
Doo - madoo
Sentensi za wastani na ukubwa
Hali ya udogo hupatikana kwa urahisi baada ya kupata ukubwa . Ukitaka kupata usogo wa nomino yoyote, utapachika ki mwanzo wa nomino ya ukubwa. Kwa hivyo: Ki + UKUBWA = UDOGO
Tazama:
Ukubwa udogo
jichwa kijichwa
jitu kijitu
toto kitoto
lango kilango
Kumbuka nomino zote za hali ya udogo huorodheshwa katika ngeli ya KI - VI.
Sentensi za ukubwa na udogo
1. Mbwa mkubwa alimkibia ng'ombe. ( andika katika ukubwa)
2. Kijoka kilichokiuma kibuzi ni hiki. ( andika katika wingi)
3. Watoto wale ni wadogo. ( andika katika ukubwa)
4. Milima yote haina miti mingi ( andika katika udogo)
5. Mtoto yule mdogo ni wa mgeni wangu. (andika katika udogo/wingi)