Utumiaji wa methali

Utumiaji wa methali katika insha.

Ni vizuri mwanafunzi aelewe kwamba, katika insha methali hutumika kwa njia mbili:

i) kuonyesha mhusika aliyazingatia mafunzo ya methali.

ii) kuonyesha mhusika aliyapuuza. Uangalie mfano ufuatao:

Mhusika fulani alikuwa na bidii katika shughuli zake. Katika mfano huu, tunaweza kutumia methali mchumia juani huliakivulini kuonyesha aliizingatia methali hii. Iwapo mhusika alikuwa mzembe bado tunaweza kuitumia methali hii huku tukionyesha aliipuuza.

 

Semi za kutumia pamoja na methali

  • Waambao waliamba ... (methali)
  • Chambilecho wahenga ... (methali)
  • Wahenga hawakukosea shabaha waliponena ... (methali)
  • Wahenga hawakututia kiwi walipoamba ... (methali)
  • Wahenga hawakutupaka mafuta kwa mgongo wa chupa waliponena ... (methali)
  • Wahenga hawakutupiga mafamba walipoamba ... (methali)
  • Wahenga hawakutuchezea kayaya za chini kwa chini waliposema ... (methali)
  • Wahenga hawakuuza upepo kwa dunia waliposema ...(methali)
  • Wahenga hawakutupatia ulimi wa kulazia waliponena ... (methali)
  • Wahenga hawakutuchezea shere walipolonga ... (methali)
  • Wahenga hawakutoa ngebe walipolonga .