Maumbo

- Katika uandishi wa insha, mwanafunzi ana uhuru wa kuumba hali fulani ili kueleza mawazo yake.

- Itazame mifano ifuatayo:

  • Ilikuwa ni sawa na kukimbizana na upepo - Jambo lisilowezekana -
  • Watu wengi wanazidi kuabiri basi la ukimwi - wanazidi kuambukizwa virusi vya ukimwi -
  • Kujaribu kupigana nao ilikuwa sawa na mwanambuzi kujaribu kupigana na kundi la fisi - kupigana na walio na uwezo zaidi ukilinganisha na wako.
  • Kutarajia huruma ilikuwa sawa na kutegemea paka amwonee panya huruma – Kutarajia mema kutoka kwa mtu katili -
  • Maisha ni vumbi litokomeapo mafuriko ya mauti yakumbapo – Tukio la ghafla la kifo.
  • Maisha ni sawa na mwanga utokomeapo giza la kifo litandapo – kuonyesha hali ya tukio la kifo. Sanasana la ghafla .
  • Kifo ni nduli mwovu – Ukatili na kifo .
  • Kujaribu kuchota maji kwa pakacha - Kufanya jambo litakalokusababishia hatari, kujitumbukiza kwenye jungu la mafuta moto. ... kujitia kinywani mwa simba ... kujitoma kwenye tanuri yenye moto ... kujipeleka pangoni mwa chatu