Insha ya siku ya michezo

Insha kuhusu siku ya michezo shuleni/kijijini/mtaani :

Mambo ya kuzingatia:

  • Mchezo upi?
  • Michezo ilikuwa wapi?
  • Michezo ilifanyika lini?
  • Timu husika zilikuwa zipi?
  • Mchezo uliendeleaje?
  • Chochote cha ajabu kilichotokea?

 

Mfano:

Mchezo shuleni

Mtiririko wa mawazo

- Kufika kwa maashiki na mashabiki.

- Kuanza kwa mchezo.

- Wachezaji kuchukua nafasi zao

- Mpuliza kipenga kuanzisha mechi.

- Mchezo kuanza na kuchezwa kwa kasi na ufundi

- Bao kufungwa/wavu kutingizwa

- Baadhi ya wachezaji kucheza visivyo

- Msaidizi wa refa kuinua kibendera

- Mkwaju wa adhabu kupigwa

- Kadi za manjano na nyekundu kutolewa na refa

- Mkwaju wa penalti

- Kipindi cha mapumziko – kwa robo saa

- Bao la kusawazisha

 

Mchezo shuleni

Mtiririko wa mawazo

- Muda wa kawaida kukatika.

- Muda wa majeruhi kuongezwa

- Kipenga kupulizwa

- wakati kukatika

- Kuongezwa kwa muda wa ziada

- Wakati wa ziada kukatika bado matokeo yakiwa sare

- Kupigwa kwa mikwaju ya penalti

- Mshindi kupatikana

- Kutolewa kwa kombe

- Baadhi ya mashabiki na maashiki kusababisha zogo na zahama

- Walinda usalama kutuliza ghasia

- Kuondoka kwa kila mtu.