Insha kuhusu wizi/uvamizi
Mambo ya kuzingatia:
- Uvamizi ulitokea wakati upi?
- Ulitokea wapi? k.m. shuleni, nyumbani, hotelini, safarini, benkini, nk.
- Hali ya uvamizi k.m. silaha zilitumiwa/damu ilimwagwa/watu waliuawa/ nk.
Mfano:
- Uvamizi nyumbani: Mtiririko wa mawazo
- Ni wakati wa usiku mchanga.
- Mnapiga soga huku mkiota moto na watu wa aila yako.
- Mvua inaendelea kunyesha.
- Ghafla mlango wa jikoni unagongwa kwa nguvu na kuvunjika.
- Watu walio na silaha kali kali wajitoma jikoni.
- Amri zinatolewa na wavamizi.
- Risasi kufyatuliwa.
- Kamsa kupigwa na baadhi yenu.
- Kujeruhiwa kwa mzazi wako.
- Wasamaria wema kufika.
- Ving’ora zaidi kupigwa.
- Askari kufika.
- Mapambano kati ya askari na wavamizi.
- Kutoroka kwa baadhi ya wavamizi.
- Kukamatwa kwa wengi wao.
- Kupelekwa korokoroni.
- Waliojeruhiwa kupelekwa hospitalini.
- Tamati.