Insha kuhusu sherehe
Mambo ya kuzingatia:
- Ilikuwa sherehe ya aina gani?
- Sherehe ilikuwa wapi?
- Sherehe ilikuwa lini?
- Sherehe yenyewe ilikuwa vipi?
Mfano:
Sherehe ya harusi:
- kurauka mapema siku hiyo.
- kujitayarisha kisha kung’oa nanga kuelekea maabadini ambapo harusi ingefanyika.
- kufika maabadini
- kushirikiana na wengine kuupamba ukumbi
- kuwasili kwa waalikwa
- kuwasili kwa maarusi
- kutembea hadi madhabahuni
- kiongozi wa dini kuanza kuongoza sherehe
- kuvishana pete na kutoa ahadi na miadi
- kutolewa kwa keki
- maombi na kwenda ukumbuni kwa viburudisho
- kutolewa zawadi na kufumukana kwa waalikwa huku maarusi wakielekea kuanza fungate yao.
Katika insha yako, unaweza kujumuisha jambo lisilokuwa likitarajiwa ili insha yako ivutie zaidi
k.m.
- Mpenzi wa kitambo kupinga harusi
- Wazazi wa upande mmoja kuipinga harusi
- Bibi harusi kukumbwa na kite cha uzazi –alikuwa mjamzito
- Wezi kuvamia wakinuia kuiba zile pete za fahari
- Wezi kukimbilia pale maabadini huku wakifuatwa na polisi, nk.
- Kiongozi wa dini kugoma kuiongoza ile shughuli kutokana na sababu alizozijua yeye mwenyewe na Mungu wake
- Veti ya bibi harusi kuchatuliwa na mwenawazimu mmoja. Kumbuka hata baada ya vioja na viroja hivi, sherehe zinaweza kuendelea kama kawaida au zitumbukie nyongo. Haya yatategemea uamuzi wako wewe mwandishi au masharti ya swali.