Mifano ya vidokezo
Mfano:
- Ajali ya barabarani.
- Mambo ya kujiuliza.
- Ulikuwa wakati upi na wewe ulikuwa wapi?.
- Ajali ilitokea wapi na lini?
Mtiririko wa mawazo:
- ulikuwa kando ya barabara ukisubiri gari kuelekea shuleni asubuhi hiyo.
- kuonekana kwa gari likija kwa kasi.
- kung’oka kwa gurudumu.
- kushikwa kwa breki.
- juhudi za dereva kutofua dafu.
- kuyumbayumba kwa gari.
- kuanguka kwa gari na kubingirika.
- kishindo kikubwa kusikika.
- watu kupiga kite.
- wasamaria wema kufika.
Mifano ya vidokezo vya insha mbalimbali
Insha kuhusu ajali
Baadhi ya ambayo maswali mwanafunzi anastahili kujiuliza:
- Ni ajali ya aina gani? k.m. Ajali ya gari barabarani, gari la moshi n.k.
- Ajali ilitokea wapi? -Ni nini chanzo cha ajabu hiyo?
- Ajali ilitokea lini?
- Wakati wa ajali, ulikuwa wapi?
- Je, ulishuhudia ajali au ulihusika?
- Ajali yenyewe ilikuwaje?
- Ni yapi yaliyotendeka pindi tu baada ya ajali?
Mtiririko wa mawazo:
- watu kuumia
- watu kutolewa garini
- wengine kufariki
- kufanyiwa huduma ya kwanza
- kukimbizwa hospitalini
- matabibu kufika kwa ambulensi
- kuendelea kuwahudumia majeruhi.
- wahasiriwa wachache kunusurika.
- hali kwa jumla: damu kutapakaa kila mahali, kilio cha uchungu: kilio cha majonzi majeruhi kuwa na nyoyo za kuku
- kufika kwa polisi
- kufanya udadisi wao
- maiti kupelekwa makafani (ufuoni)
- watu kutawanyika. Kumbuka unaweza kutaja jambo ambalo halikutarajiwa katika mazingira yale ili insha yako ivutie zaidi. k.m. Baadhi ya watoaji huduma za kwanza kugunduliwa wakiwaibia majeruhi na hata waliokufa.