- Insha ya picha huandikwa kutokana na picha au michoro iliyotolewa. Katika insha ya aina hii, mtahiniwa huwa amepewa picha/michoro kadhaa.
- Mtahiniwa basi hutakikana kutunga insha yake kutokana na picha/michoro ile. Sharti insha atakayotunga ilingane na mawazo yaliyonuiwa kuwasilishwa kupitia picha/michoro ile.
Mambo muhimu ya kuzingatia:
- Mtahiniwa asirejee picha/ michoro moja kwa moja aandikapo insha yake k.m. ni makosa kusema, “Katika picha /mchoro wa kwanza, pana mtu anayeendesha gari kwa kasi...” Insha ya picha hadithi ni kama insha hizi nyingine. Tofauti ni kuwa, mtahiniwa huongozwa na picha / michoro kuiandika insha yake.
Zoezi
Andika insha ukizingatia mfululizo wa picha hizi (A-E)