Insha ya mjadala
- Katika insha ya aina hii mtahiniwa hupewa hoja fulani. Hutakiwa kuiunga mkono au kuipinga. Ni uamuzi wa mtahiniwa kuunga mkono hoja hiyo au kuipinga hoja ile.
- Iwapo ataamua kuiunga mkono hoja fulani ni lazima aonyeshe uzuri wake huku akionyesha ubaya au udhaifu wa upande huo mwingine.
Uandikapo insha ya aina hii, lazima uyazingatie yafuatayo.
- Utangulizi – Utaonyesha msimamo wako. Hivi ni kusema, utaeleza unaunga mkono upande upi.
- Mwili: utatetea uamuzi wako. Hivi ni kusema utaonyesha uzuri wa swala unalounga mkono huku ukionyesha kasoro za swala ulipingalo.
- Tamati: Utasisitiza uamuzi wako wa kuiunga mkono au kupinga hoja husika huku ukiwapatia watu changamoto ya kubadili mawazo yao na kukuunga mkono.
Mifano:
MAISHA YA MASHAMBANI NI BORA KULIKO YA MIJINI. Jadili.
Mambo ya kuzingatia: -
- Usafi wa mazingira. -
- Msongamano wa watu. -
- Ushrikiano baina ya wakazi. -
- Upatikanaji wa huduma kama vile usafiri, mawasiliano, shule, vyoo, hospitali n.k. -
- Uhalifu. -
- Maadili ya jamii. -
- Kiwango cha ubora wa maisha. - Maji safi, stima n.k. -
- Gharama ya maisha. -
- Kiwango cha utegemeaji baina ya watu n.k.
SHULE ZA BWENI NI BORA KULIKO ZA KUTWA: Jadili.
Mambo ya kuzingatia; -
- Wakati wa kutosha wa kusoma. -
- Mazingira shwari ya kusomea. -
- Matatizo ya kijamii. -
- Ukosefu wa mahitaji. -
- Matatizo ya usafiri. -
- Mabadiliko ya hali ya hewa k.m. mvua. -
- Mito kufurika na daraja kuharibiwa n.k. -
- Uhusiano wa kijamii –
- Kuwa karibu na watu wa jamii – kuwakosa n.k.
Zoezi
Andika insha za mjadala ukizingatia mada zifuatazo:
- Heri kufa njaa kuliko kuiba. Jadili
- Elimu ya msichana ni bora kuliko ya mvulana. Jadili.
- Wanawake na wanaume wote wanastahili kuwa sawa. Jadili
- Elimu ni bora kuliko mali. Jadili.
- Teknolojia imeleta hasara kuliko faida. Jadili.