Walemavu |
---|
Maswali kadirifu |
1. Mtu aliye na dosari kwenye viungo vya mwili huitwa _____.
2. Mtu aliyepofuka jicho huitwa _____.
3. Mtu aliyepofuka macho yote mawili huitwa ______.
4. Mtu asiye na meno yote kinywani huitwa ______.
5. Mtu aliye na meno machache kinywani huitwa _____.
6. Mtu aliyezaliwa na meno huitwa _____ au ______.
7. Mtu anayezungumza na ncha ya ulimi huitwa _____ au _____.
8. Mtu aliye katika kidole huitwa _____.
9. Mtu aliyevia huitwa _____.
10. Mwanamke asiyeweza kuzaa huitwa _____.
11. Mwanaume asiyesimika au ambaye jogoo lake haliwiki huitwa _____.
12. Mtu asiye kuwa na rangi kamili ya ngozi huitwa _____.
13. Mtu hasa mtoto anayetabawali kwenye malazi huitwa _____.
14. Mtu aliye na meno yaliyopandana kinywani huitwa _____.
15. Mtu aliyepindika miguu kama uta huitwa _____.
16. Mtu asiyeweza kuongea huitwaje _______.
17. Mtu asiyeweza kusikia huitwa ________ au ________.
18. Mtu aliyekatika nyama za pua huitwa _______.
19. Mtu aliyekatika nyama za ndewe huitwa _________.
20. Mtu anayeongea/zungumza kwa kusitasita au kudodosa maneno huitwa ______ au _______.
21. Mtu asiye na nywele kichwani huitwa _______.
22. Mtu ambaye nywele zake hung'oka ovyoovyo huitwa _______ au _______.
23. Mtu aliye na nundu mgongoni huitwa ______, ______, ______, ______, _______ au _______.
24. Mtu aliyepindika vidole vya miguu au mikono huitwa _______.
25. Mtu aliyekatika mkono huitwa ________.
26. Mtu aliyekatika vidole huitwa ________.
27. Mtu aliye na mguu mmoja huitwa _______.
28. Mtu aliyelemaa miguu yote miwili na anatembea kwa kusota au kukweta huitwa ________.
29. Mtu mfupi kimaumbile huitwa _______, ______, ______, ______ au ______.
30. Mtu ambaye miguu yake imepindika nje huitwa ________.
31. Mtu ambaye amepindika miguu yake kwa ndani huitwa _______.
32. Mtu aliye na miguu iliyopindika kama uta huitwa ______.
33. Mtu aliye na meno yaliyopandana kinywani huitwa ________.
34. Mtu anayezungumza kwenye pua huitwa kipua au ________.
35. Mtu mwenye viungo vyote vya uzazi cha kiume na kike huitwa ________.
36. Mtu hasa mtoto anayetabawali kwenye malazi huitwa _________.
37. Mwanamume asiyekuwa na mbegu za uzazi huitwa _________.
38. Mwanamke asiyeweza kuzaa huitwa __________.
39. Mtu asiyekuwa na rangi kamili ya ngozi huitwa _________.
40. Mwanamume asiyesimika au ambaye jogoo lake haliwiki huitwa ___________.