Viashiria na viulizi pamoja na ngeli by
Viashiria ni nini?
Viashiria ni kivumishi kinachotumiwa kuonyesha kwa kutegemea mahali kulipo kitu kinachoonyeshwa aidha huitwa kionyeshi.
Aina ya viashiria
- Kiashiria cha karibu - HAPA
- Kiashiria cha mbali kidogo - HAPO
- Kiashiria cha mbali sana - PALE
MIFANO KATIKA SENTENSI
- Mbuzi huyu ni mnono kuliko yule.
- Mbuzi hawa ni wanono kuliko wale.
- Kiu chako hicho si kama chake.
- Embe lile linafanana na hilo.
- Maembe yale yanafanana na hayo.
ZOEZI
- Giza ____ (hilo,hiyo,hicho,huo) lilitutisha,
- Nitakupa vifaa ____ (zako, vyako,yako, chako) sasa hivi.
- uji ____ (yake, wake, lake, zake) umemwagika.
- Amechukua kuni ____ (yake, zake, chake, kwake) akaenda
- Nyumbani ____ (zile, yale,pale,ile) hupendeza.
- kusafiri ____ (yake, wake, zake, kwake) kulimfurahisha.
MAJIBU
- HILO
- VYAKO
- WAKE
- ZAKE
- PALE,
- KWAKE