6
Wana tofauti gani?
Lepe la usingizi : usingizi wa muda mfupi.
Kuwaza na kuwazua : kufikiri sana
Vifijo na vigelegele : kelele za shangwe.
Mhebi : sahibu, rafiki
Karimu : kinyume cha mchoyo.
Kuazima : kumpa mtu kitu atumie na kukirejesha baadaye.
Kudai : kuitisha kitu
Siku moja sungura alimwalika rafikiye kwenye arusi ya bintiye korongo.
Jongoo alifurahishwa sana na mwaliko huo naye akaamua kuhudhuria.Kwa bahati baya hakuwa na miguu ya ku chezea ngoma huko arusini.Usiku kucha hakupata hata lepe la usingizi kwa kuwazana kuwazua.Alikuwa na shauku sana kwennda lakini hakupata jawabu.Baada ya kufikiri sana aliamua kwenda kuazima miguu kutoka kwa rafikiye nyoka.
Alimpata amelala chini ya mti mkubwa mawindoni «Mhebi nyoka, nimealikwa kwenye harusi na rafiki yangu sungura lakini kama ujuavyo siwezi kuhudhuria harusi hiyo kama sina Miguu.Nakusihi uniazime miguu yako kwa muda ili niweze kuhudhuria harusi hii.Nakuahidiyakwamba nitakurudishia miguu yako mara tu nirudipo kutoka hafusini.
Nyoka ambaye alikuwa karimu sana alimwazima huku akimwambia«Usiwe na wasiwasi rafiki, nitakuazima miguu yangu lakini ni sharti uhakikishe utanirejeshea mara tu harusi imalizikapo”
Jongoo alifurahi sana kupata miguu akaipachika mwilini mwake nakutembea wima wima akielekea nyumbani kwake huku akimshukuru nyoka.Huko nyuma nyoka alilala kifudifudi akimwa ngalia jongoo jinsi alivyotembea kwa maringo kama tausi.
Siku ya harusi alipofika nyumbani kwa sungura wageni wote walimwangalia sana na kumwajabia alivyo kuwa mrembo.
Walimshangilia kwa vifijo na vigelegele.Karamu iliendelea vizuri na baadaye mlo vinywaji na ngoma za makao,jongoo alishika njia kurudi nyumbani kwake akiandamana na binamuye tandu.
Tandu alimwomba binamuye jongoo amgawie baadhi ya miguu yake.Hakumkatalia binamuye haja yake hivyo basi waliketi chini ya mukuyu na kugawana ile miguu ya nyoka lakini jongoo alijibakizia miguu mingi zaidi.
Siku nyingi zilipopita bila nyoka kurejeshewa miguu yake ,alishikwa na wasiwasimwingi kwani hakujua madhara yaliyompata rafikiye.
Nyoka aliamua kwenda kuchungua ni jambo gani lililompata jongoo hata akakosa kutimiza ahadi yake lakini hakuwa na miguu.
Kutoka siku hiyo ,nyoka angali akitambaa chini akifikiri atakavyofika nyumbani kwa jongoo kudai miguu yake.Naye jongoo bado angali na ile miguu ya nyoka na kila mara anapohisi kuwa nyoka yu karibu naye, hutoroka na kumwepa.Aidha tandu binamuye humwepa nyoka vilevile mpaka wa leo.
1.Ni nani hakuwa na miguu
2Ni binti ya nani aliyekuwa anaolewa?
3Jongoo aliazimwa miguu na nani?
4Binamuye jongoo aliitwa___.
5Arusi ilisababisha hasara gani kwa nyoka?
6Hadithi hii ina funzo gani?
7.Kwa nini jongoo hutoroka anapohisi nyoka yu karibu?
1Hakuwa na miguu.
2Ni binti ya sunguura alikuwa akiolewa.
3Alizimw na nyoka.
4Aliitwa tandu.
5 Arusi ilisababisha nyoka kupoteza miguuyake
6Tusiamini watu sana.
7Jongoo hutoroka kwa sababu alikataa kumrejeshea nyoka miguu yake.