Tarakilishi by
Pius Mungai
6
MALENGO
Kufikia mwisho wa funzo mwanafunzi aweze kueleza maana ya tarakilishi Maana ya tarakilishi...
Tarakilishi ni kifaa cha kielektroniki cha kuhifadhi, kukokotoa na kuchanganua taarifa zilizoingizwa pamoja na kuongoza mitambo mbalimbali.
Tarakilishi pia huitwa Kompyuta
Sehemu za tarakilishi
Tararakilishi huwa katika ngeli ya I-ZI
Tarakilishi ina sehemu tofauti tofauti
(a)kitengokikuu cha uchakataji
(b)Kipanya
(c)kiwambo au mulishi
(d)Bodidota au bodiyadota
Maswali
- Eleza maana ya kompyuta
- Taja sehemu nne za kompyuta
Majibu
- Tarakilishi ni kifaa cha kielektroniki cha kuhifadhia, kukokotea, na kuchanganua taarifa zilizoingizwa pamoja na kuongoza mitambo mbalimbali.
- kipanya ,bodibota,mulishi, kitengo kikuu cha uchakataj.