Mahakamani |
---|
Maswali kadirifu |
- Mahakamani ni mahali ambapo kesi na mashtaka mbalimbali huamuliwa. Pia huitwa kortini.
1. Hakimu/jaji – Huamua kesi au hutoa hukumu.
2. Mshtaki - aliyeleta malalamiko mahakamani
3. Mshtakiwa - anayedaiwa au kufikiriwa ndiye mwenye kosa.
4. Shahidi - anayetoa ushahidi. Aliyeona au kusikia tukio husika.
5. Wakili - Anayemtetea mshtaki au mshtakiwa.
6. Kiongozi wa korti (Mashtaka) – Anayemwongoza shahidi kutoa ushahidi. (Anayeongoza na kuelekeza mkondo wa kesi mahakamani)
7. Karani wa korti – Anayeandika matukio kortini (Anayeshughulikia barua na rekodi za kesi kortini)
8. Mshukiwa – anayedhaniwa kuwa amehusika katika uhalifu fulani.
9. Mahabusu – aliyehukumiwa kifungo gerezani/jelani.
10. Hakimu mkazi – hakimu anayeshughulikia mahakama fulani.
11. Mkuu wa sheria – mshauri mkuu wa serikali kuhusiana na mambo ya sheria.
12. Kiongozi wa mashtaka – wakili wa kuendesha na kuongoza mashtaka mahakamani.
13. Mdai – mlalamishi. Mtu anayepigania haki yake kutoka kwa mdaiwa.
14. Mdaiwa – mtu anayetakiwa alipe au arejeshe kitu cha mwingine.
15. Mtuhumiwa – mshukiwa anayefikiriwa amefanya kosa.
16. Kesi ya jinai – kesi iliyo na uzito mkubwa k.m. kesi ya mauaji.
17. Kesi ya uhaini – kesi kutokana na kupanga njama za kupindua serikali.
18. Ithibati – vitu vinavyowekwa au kutolewa mahakamani kama sehemu ya ushahidi.
19. Ahirisha kesi – kutangaza kesi isikilizwe siku au wakati mwingine.
20. Hatia – kosa linalostahili adhabu. (kosa mtu apatikanalo nalo).
21. Daawa – kesi dhidi ya mtu mmoja na mwengine.
22. Kuruka kesi – kukataa kukabiliana na mashtaka.
23. Kukata kesi – kutoa hukumu- kuamua kesi; kutangaza matokeo ya kesi.
24. Kata rufani – kuomba kesi isikilizwe upya.
25. Dhamana – malipo yanayotolewa na mshtakiwa ili aachiliwe huru kesi yake inapoendelea.
26. Faini – fedha inayotozwa kuwa ni adhabu kwa mwenye hatia.
27. Kizimba – sehemu katika korti anamokaa mshtakiwa, mshtaki au shahidi.
28. Hukumu – uamuzi katika kesi.
29. Korokoro – seli ya kufungia washukiwa katika kituo cha polisi.
30. Rumande – sehemu maalum katika jela wanapowekwa mahabusu ambao kesi zao hazijakamilika.
31. Jela – Sehemu ya kufungia mahabusu wanapotumikia kifungo chao.
32. Pingu/vikuku – vyuma aghalabu vya duara vya kufungia wahalifu hususan mikononi.