Mahakamani |
---|
Maswali kadirifu |
1. Mahali ambapo kesi huamuliwa huitwa _____.
2. Kukata rufani ni kufanya nini?_____.
3. Hakimu wa mahakama za kislamu huitwa _____.
4. Anayetoa uamuxi wa kesi mahakamani za Kiislamu huitwa ____.
5. Kesi ya jinai ni gani?
6. Nini maana ya mahabusu?
7. Daawa ni kesi sampuli gani ?
8.Anayeongoza mashtakaa kortini huitwa _____.
9. Washukiwa mara nyingi huachiliwa kwa _____ wakati kesi inapokuwa ikiendelea.
10. _____ ni uamuzi katika kesi.
11. Shahidi ni nani?
12. Shahidi husimama wapi anapotoa ushahidi mahakamani?
13. Uamuzi wa kimahakama huitwaje? _____.
14. Kisawe cha mahakamai ni _______.
15. Tofautisha hatia na dhambi.
kiongozi wa mashtaka, husuni, kizimbani, dhamana, ithibati, wakili, rumande; shahidi, faini, korokoro.
1.Katika kesi hiyo, askari walileta pombe haramu iliyonaswa kama _____.
2. Mshtakiwa alipopatwa na hatia, alihukumiwa kutoa ______ ya shilingi elfu tano.
3. Licha ya kutetewa na ______ wake, mshtakiwa hakuepuka kifungo gerezani.
4. Ilimbidi mshukiwa apelekwe rumande aliposhindwa kulipa _____.
5. Mshtakiwa alitulia pale _________ alipoyasikiliza mashtaka yakisomwa.
6. Atoaye ushahidi mahakamani huitwa ________.
7. _____________ huongoza mashtaka dhidi ya mshukiwa.
8. Chumba cha kufungia mshukiwa katika kituo cha polisi ni ______.
9. Mahabusu hutumikia kifungo chake katika _________
10. Mshtakiwa alipokataa mashtaka, aliamriwa arudishwe ____ kwa wiki mbili.