Viungo vya mwili |
---|
Maswali kadirifu |
- Mwili wa binadamu unavyo viungo tele.
- Kila kiungo kina kazi yake na ni lazima vyote vishirikiane ili mwili uwe katika hali nzuri.
1. Ulimi – kiungo cha kuonjea, kilicho ndani ya mdomo.
2. Meno – hutafunia chakula.
3. Ufizi – nyama iyashikiliayo meno.
4. Utaya – mfupa unaoyashikilia meno.
5. Koromeo/umio – mfereji unaotumikia kuteremshia chakula au kinywaji hadi tumboni. Kifuko kinachotolea mate.
6. Tumbo – sehemu ya kupokea chakula na kuanza kukisaga.
7. Uchanga/uchengele/chango – utumbo mwembamba wa kupitishia chakula kilichosagwa.
8. Moyo/mtima – kiungo kisukumacho damu ili ienee mwilini.
9. Mshipa – mrija au mfereji mdogo unaopitisha damu na pia fahamu katika mwili wa kiumbe.
10. Neva – mishipa ya fahamu mwilini. 11. Ateri– mshipa mkubwa uchukuao damu kutoka moyoni. 12. Pafu – kiungo kinachotumika kusafishia hewa. Hutoa hewa chafu na kuingiza hewa safi mwilini.
13. Figo/ buki/nso – kiungo cha umbo la haragwe kisafishacho damu.
14. Ini – kiungo kitiacho nyongo; kiungo kinachobadilisha glukozi kuwa glukojeni; kiungo kinachopima kiwango cha sukari katika damu.
15. Kongosho – kiungo kinachotoa dawa ya kusawazisha damu; kiungo cha kusawazisha sukari kwenye damu.
16. Wengu/bandama– kiungo kitoacho dawa ya kusaidia kusagia protini kwenye chakula.
17. Nyongo – majimaji machungu ambayo hutengenezwa na ini na hutumika kuyeyushia chakula tumboni.
18. Ubongo – sehemu laini kichwani iliyo na mishipa ya fahamu.
19. Fuvu la kichwa – mfupa mgumu ufunikao ubongo.
20. Kibofu – kifuko cha mkojo kilichopo tumboni.
21. Kitefute – mshipa wa shavuni.
22. Kapilari – mishipa midogo ya damu inayosambaa mwilini.
23. Vena – mshipa urejeshao damu moyoni kutoka sehemu mbalimbali za mwili.
Tazama picha hii.