Kilimo |
---|
Maswali kadirifu |
- Kilimo pia huitwa zaraa.
Yafuatayo yanahusiana na kilimo.
1. Shamba/konde – sehemu itumiwayo kukuzia mimea.
2. Kichaka – sehemu iliyo na miti na nyasi. Sehemu isiyolimwa.
3. Weu/ucheu – sehemu ya ardhi iliyolimwa kwa kupanda.
4. Kwekwe/magugu – nyasi na mimea iliyoota pasi kupandwa na huathiri mimea mingine ambayo imepandwa.
5. Makoongo – mashimo au mitaro ya kupandia mbegu au miche.
6. Miche – mimea michanga.
7. Kituta/kitangu – sehemu ya kukuzia miche kabla haijapandwa.
8. Kuo – Mstari wa miche
9. Kitalu – sehemu ya kukaushia mbegu.
10. Ghala – sehemu ya kuhifadhia mavuno hususan nafaka kavu k.v. mahindi.
11. Kufyeka – kukata na kuondoa nyasi na miti.
12. Kung’oa visiki – visiki ni sehemu ya chini za miti; sehemu ya shina na mizizi. Kwa hivyo kung’oa visiki ni kuziondoa ardhini sehemu hizo.
13. Kulima muauta – kulima huku ukiinua matuta ya udongo juu.
14. Kulima sesa – kulima huku ukilainisha udongo.
15. Kupalilia – kulima huku uking’oa kwekwe na magugu.
16. Kutayarisha makoongo – kutayarisha mashimo au mitaro ya kupandia mbegu au miche.
17. Kupanda sia – kupanda mbegu bila kutayarisha makoongo/mashimo.
18. Kupandikiza/atika – kuung’oa mche na kuupanda sehemu nyingine.
19. Kupogoa – kuyakata na kuyapunguza matawi ya miti.
20. Kunyunyizia – kumwagilia maji kwa utaratibu.
21. Kuvuna/kuchuma – kutoa mazao ya mimea shambani.
1. Maksai - ng’ombe dume aliyehasiriwa na hutumiwa kuburutia plau.
2. Mbuguma - ng’ombe anayeendelea kuzaa.
3. Njeku - ng’ombe dume ambaye bado hajawa fahali.
4. Ndenge - mbuzi dume mchanga.
5. Beberu - mbuzi dume.
6. Mori - ng’ombe jike ambaye bado hajazaa.
7. Mtamba/mfarika/dacha - mnyama wa kike ambaye amekomaa lakini hajazaa.
8. Jogoo/jimbi - kuku wa kiume aliyekomaa.
9. Koo/mtetea - kuku wa kike ambaye amekomaa.
10. Tembe - kifaranga wa kike.
11. Pora - kifaranga wa kiume.
12. Kiweto - koo asiye na uwezo wa kutaga mayai.
13. Kutaga - kutoa yai kutoka kwenye kiloakia.
14. Kuatamia - kalia au lalia mayai kama afanyavyo kuku ili yaanguliwe.
15. Angua/totoa - toa vifaranga ndani ya mayai.
16. Kunyonyoa - kuondoa nyoya za kuku.
17. Pepea - weka matunda palipo na joto ili yaive.
18. Yai viza - yai bovu lisiloweza kuanguliwa.
19. Kiangulio/kitotoa - mtambo wa kuangulia mayai ya kuku.
Kifaa
|
Kazi |
Fyekeo | Kufyekea nyasi |
Jembe | Kuchimbia ardhi, kulimia. |
Panga | Kukatia miti, kuni. |
Reki | Kuburura majani, kusawazisha udongo. |
Haro | Kulimia. |
Mundu | Kukatia miti. |
Sepetu | Kuchotea mchanga. |
Dodoki | Kusugulia mwili wakati wa kuoga. |
Tingatinga | Kukokota vitu. |
Glovu | Kukingia mikono. |
Shoka | Kupasulia kuni. |
Plau | Kulimia. |
Pigi | Kuangulia matunda. |
Panga
Fyekeo
Jembe
Sepetu
Plau
Reki
Shoka