Zana za vita |
---|
Maswali kadirifu |
Hizi ni silaha zitumikazo wakati wa vita.
1. Jeti: eropleni iendayo kwa kasi sana. Inatumika kupeleleza na hata kudondosha mabomu.
2. Bomu: silaha ambayo hulipuka na kuleta maafa makubwa.
3. Bunduki: silaha itumiwayo kufyatulia risasi.
4. Bastola: bunduki ndogo. Hushikwa na kufyatulia risasi kwa mkono mmoja.
5. Mzinga: silaha iliyo na mwanzi mkubwa ambao hutumiwa kurushia risasi. Ina nguvu kuliko bunduki.
6. Nyambizi/sabmarini: chombo cha kivita ambacho husafiri chini ya maji.
7. Manowari: meli ya kivita.
8. Kifaru: chombo mfano wa gari la chuma ambacho hutumika kwa vita.
9. Helikopta za kijeshi: eropleni iliyo na uwezo wa kutua popote. Huwa na panka juu.
10. Magari ya deraya: magari yawezayo kusafiri katika barabara mbovu na kwa kasi.
11. Dereya/dirizi: nguo za vita zilizotengenezwa kwa chuma.
12. Parange: silaha mfano wa panga iliyo na makali upande uliopinda.
13. Korofindo: bunduki ya kushindilia gobori.
14. Panga: silaha mfano wa kisu.
15. Singe: kisu kinachochomekwa/kinachowekwa katika mtutu wa bunduki.
16. Sime: jisu lenye makali pande mbili.
17. Mkuki: silaha iliyochomekwa chuma ambacho kimechongoka.
18. Mshale: kijiti na chembe na hurushwa kwa upinde.
19. Kombeo/teo/kumbwewe: chombo cha kurushia mawe.
20. Guruneti