Vyombo mbalimbali |
---|
Maswali kadirifu |
Tumia haya maneno.
Bikari, panka, bilula, taipureta, jenereta, mtaimbo, milizamu, kitindio, panchi, kifyonzavumbi, uyoka, kamera, winchi, swichi, pantoni.
1. Chombo cha kutobolea mashimo karatasini ni ___________.
2. Chombo cha kutilia kisu makali ni ___________.
3. Chombo cha kuvunjia mawe na kuinulia vitu ni ___________.
4. Chombo cha kufungia au kufungulia maji mferejini ni ___________.
5. Mashine ya kuonyeshea vitu vilivyomo ndani k.v. chembe za mwili ni ___________.
6. Ufagio wa umeme utumiwao kwenye mazulia ni ___________.
7. Kifaa kidogo cha kunyofolea ndevu ni ___________.
8. Mashine madogo ya kutolea maandishi ni ___________.
9. Chombo cha kupigia picha ni ___________.
10. Mtambo wa kutoa nguvu za umeme ni ___________.
11. Mtambo wa kuinulia mizigo mizito ___________.
12. Chombo cha majini cha kuvushia mizigo, watu n.k___________.
13. Kifaa cha chuma kizungukacho na kule•ta ubaridi ___________.
14. Kifaa kinachotumika kuzima au kuanzisha mkondo wa umeme kusambaa kwenye waya ___________.
15. Chombo cha kuchorea duara katika hesabu za maumbo ___________.
1. Timazi
2. Msumari wa hesi
3. Pimamaji
4. Chenezo
5. Tumbuu
6. Pishi
7. Spana
8. Mtaimbo
9. Mizani
10. Mvukuto