Utangulizi |
---|
Mifugo |
Wanyamapori |
Viumbe vya majini |
Ndege/Nyuni |
Maswali kadirifu |
1. Heroe/ Flamingo - ndege wa jamii ya korongo anayepatikana sehemu zenye maziwa, mwenye miguu mirefu myekundu, shingo ndefu na mwili wa rangi nyeupe wenye wekundu.
2. Mbuni - ndege mkubwa mwenye miguu mirefu na shingo ndefu ambaye hawezi kuruka ila hukimbia kasi sana.
3. Kasuku - Ni ndege mwenye rangi nyingi anyeweza kuiga maneno yanayosemwa na binadamu.
4. Chiriku - Ni aina ya ndege mdogo mwenye kelele nyingi.
5. Keremkeremu - Ni ndege mla asali.
6. Kereng’ende - Ni ndege mwitu ya jamii ya kuku lakini mmdogo mwenye rangi ya hudhurungi na miguu nyekungi.
7. Hudihudi - Ni aina ya ndege mdogo wa jamii ya njiwa mwenye mdomo mrefu na mwili wenye mistarimistari aliyemwambia Suleiman habari ya kuweko kwa Malaika wa Sheba.
8. Hondohondo - Ndege mkubwa kiasi mwenye rangi nyeusi na nyeupe na mdomo mkubwa mwekundu uliopinda.
9. Kanga - Ni ndege wa porini anayefanana na kuku mwenye mwili wa madoamadoa meupe na kichwa chenye upanga juu yake.
10. Njiwa/hua - Ndege ya jamii ya tetere au pungi lakini mkubwa anayekula nafaka mwenye rangi ya kijivu na nyeupe iliyopauka.
11. Kijimbimsitu (avuaye samaki baharini) - Ndege anayepata chakula chake kwa kupiga mbizi baharini na kukamata samaki.
12. Koleamiti
13. Tai - Ndege mkubwa mwenye mdomo uliopinda nchani, kucha ndefu zilizokunjika na kali ambaye hula mizoga na wanyama wadogo kama panya.
14. Tetere - Ndege mdogo mithili ya njiwa na wa rangi ya kijivujivu mwenye alama kama ya pete shingoni.
15. Korongo - Aina ya ndege mwenye shingo na miguu mirefu anayependa kuishi sehemu zenye maji.
16. Mwewe - Ni aina ya ndege wa jamii ya tai ambaye hukamata vifaranga na kuku.
17. Bata - Ndege mkubwa kuliko kuku anayeishi porini au anayefugwa mwenye vidole vilivyounganishwa na vingozi vyembamba vinavyomwezesha kuogelea
18. Ngojamaliko - Ndege mkubwa mweusi mwenye tamvua jekundu shingoni anayependa kula nyoka na ambaye anafanana na korongo.
19. Bumu/bundi - Ndege mkubwa mwenye macho makubwa anayeruka usiku na hulaaniwa kuleta msiba.
20. Koho - Tai mla samaki.
21. Koikoi - Ndege mkubwa mwenye shingo ndefu, miguu mirefu na anyeishi karibu na maji.
22. Komakangi
23. Pwaju - Ndege wa kahawia na kijani wa jamii ya mlembe mwenye kisuzu na mkia mwembamba.