Utangulizi |
---|
Mifugo |
Wanyamapori |
Viumbe vya majini |
Ndege/Nyuni |
Maswali kadirifu |
1. Papa - samaki mkubwa kuliko samaki wote bararini,mwenye ngozi ngumu ya kijivu, meno makubwa makali anayekula watu.
2. Nyangumi - mnyama mkubwa wa bahari mwenye umbo kama la samaki, mwenye mafuta mengi na hunyonyesha kama wanyama wengi.
3. Dagaa - Samaki wa rangi ya fedha wenye umbo dogo sana ambao hawawezi kukua zaidi.
4. Chaza - Kidudu kinachoishi ndani ya kombe.
5. Koche - kiumbe wa baharini mwenye gamba gumu jeusi, mwili mrefu uliogawanyika sehemu sehemu, miguu minane na mikono miwili yenye makucha ya kushikia ambaye anapopikwa gamba lake hubadilika na kuwa jekundu.
6. Taa - samaki mkubwa wa baharini mwenye umbo bapa na mkia mwembamba mrefu.
7. Mkunga - samaki mwenbamba mrefu mwenye umbo la nyoka ambaye ni mweusi au wa kijivu, kahawia ay mabatobato.
8. Kambare - samaki wa maji baridi mwenye kichwa kikubwakigumu cha bapa na masharubu marefu.
9. Pweza - mnayama wa baharini mwenye mikia minane.
10. Mamba - mnyama wa jamii ya kenge lakini mkubwa zaidi ambaye ana magamba na huishi kwenye maji.
11. Kiboko - mnyama mkubwa anayeishi mitoni au katika maziwa na mabwawa mwenye masikio madogo, meno makubwa na mapana na pua pana yenye mianzi mipana.
12. Chuchunge - aina ya samaki mwembamba na myenye mdomo mrefu; mchumbururu.
13. Kamba - mnyama mdogo wa baharini mwenye magamba laini na miguu mingi ambayr huliwa.
14. Nguru - samaki mkubwa mrefu mwenye kivimbe cha duara na rangi ya kijivu aishiye baharini.
15. Chewa - aina ya samaki mweusi mwenye mabaka na kinywa kipana.
16. Sangara - samaki wa maji baridi, wa jamii ya perege aliye na umbo kubwa na mdomo mpana.
17. Kangu - samaki wa aina ya pono mwenye magamba makubwa.