Viumbe wa kike na kiume |
---|
Maswali kadirifu |
Linganisha kinyume cha jinsia ya neno katika (i) kutoka (ii) (i)
Sehemu (i)
1. Baba 12. Fahali
2. Kaka 13. Mvuli
3. Mjomba 14. Njeku
4. Amu 15. Jogoo
5. Mgumba 16. Pora
6. Mtwana 17. Binamu
7. Bin 18. Babakambo
8. Shaibu 19. Mlamu
9. Kapera 20. Babu 1
10.Kungwi 21. Mwinyi
11.Ndenge 22. Mjane
Sehemu (ii)
a) Nyanya l) Mori
b) Kijakazi m) Koo/mtetea
c) Banati n) Ajuza
d) Nana o) Mtamba
e) Nina p) Mwanamwali
f) Binti q) Dada
g) Mfarika r) Halati
h) Nyakanga s) Mfaruku
i) Wifi t) Bintiamu
j) Tembe u) Shangazi
k) Mamakambo v) Tasa
Jaza neno mwafaka ili kukamilisha jozi.
Mfano: Mkemwenza ni kwa mwanyumba kama vile mjomba ni kwa shangazi
1. Mseja ni kwa ____ kama vile mtanashati ni kwa ______.
2. Tembe ni kwa _____ naye ______ ni kwa jimbi.
3. Mfalme ni kwa ________ naye Rais ni kwa _______.
4. Babu ni kwa ______ naye bamkwe ni kwa _______.
5. Kapera ni ______ kama vile ______ ni kwa kitwana.
6. Amu ni kwa _______ kama vile _______ ni kwa binti.
7. Fahali ni kwa ________ kama vile Litazame jedwali lifuatalo gumba ni kwa _______.
8. Bwana arusi ni kwa ______ kama jvile Mama Baba _____ ni kwa binti.
9. Ajuza ni kwa ______ kama vile wifi ni kwa _______.
10. Mume ni kwa _______ kama vile _______ ni kwa mama.
Taja vinyume vya majina yafuatayo.