Maliasili ya taifa |
---|
Maswali kadirifu |
- Maliasili ni vitu vinavyotokana na maumbile.
- Mifano: misitu, maji, madini n.k.
- Aghalabu, maliasili ya nchi huchangia katika utajiri wa nchi husika k.m.
- Afrika kusini imenawiri kiuchumi kutokana na utajiri wa madini.
Maliasili Matumizi / maelezo
Dhahabu. Madini yenye thamani kubwa. Ni ya rangi ya manjano mbivu. Hutengenezea mapambo.
Fedha. Madini ya rangi ya bati. Hutengenezea sarafu.
Shaba. Ni ya rangi nyekundu au nyeupe. Hutengenezea nyaya za umeme.
Almasi. Madini magumu yaliyo na thamani sana. Hukatia vioo na madini mengine.
Alumini. Madini mepesi rangi ya kijivu na fedha. Hutengenezea kikaango.
Zinki/ferasi. Madini meupe na samawati. Hupakwa juu ya mengine ili kuzuia kuota.
Chuma. Madini ngumu. Hujengea na kuundia vitu.
Risasi. Yana rangi ya buluu na kijivu hafifu. Huyeyuka rahisi kwa kuchomwa. Hutengenezwa vitu vya vioo na ngamba za sanaa
Zebaki. Majimaji na rangi ya fedha au nyekundu. Hutumiwa kupika na kuendesha mitambo.
Makaa ya mawe. Huchimbwa chini ya ardhi. Meusi. Hutumiwa kupika na kuendesha mitambo.
Chumvi. Madini meupe. Hutiwa kwenye chakula ilikuongezea ladha
Magadi. Chumvi chungu. Hutengenezea sabuni. Hulainisha chakula wakati wa kupika.
Ulanga. Meupe kama ngamba zilizoshikana. Huchimbwa ardhini.Hutengenezea vitu vya vioo na ngamba za sanaa.
Chokaa. Unga mweupe unaotumiwa kujengea, kupaka kuta za nyumba.
Bati. Meupe kidogo. Hufanana na risasi. Ni magumu
Urani. Madini mazito. Rangi nyeupe na ya fedha. Huzalisha nguvu za nyukilia.
Magnesia. Madini meupe. Hutumiwa kutengeneza dawa za kutibia kiungulia. Huchanganywa na madini mengine na hutumika kutengenezea ndege.
Aloi. Hupatikana kwa kuchanganya madini mawili au zaidi. Hutumika kutengenezea mataa ya kuongozea magari katika mizunguko ya barabara.
Jasi. Jiwe laini la chokaa. Hutengenezea saruji.
Manganizi. Madini ya kijivu na meupe. Huvunjika rahisi. Hutengenezea vioo.