Jikoni
- Jikoni ni mahali mwa upishi.
- Jikoni munaweza kuwa katika shule, nyumba au hata katika hoteli.
Msamiati wa jikoni
- Jiko – chombo cha kupikia. Jiko linaweza kuwa la makaa, kuni, stima, mvuke, gesi na hata la jua.
- Seredani – jiko la makaa.
- Mafiga/mafya – mawe matatu ya jiko la kuni.
- Dohani – mfereji wa kutolea moshi jikoni.
Aina za jiko
- Uchaga – sehemu ya kuwekea kuni.
- Karo – sehemu ya jikoni ya kuoshea vyombo.
- Mwiku/kiporo/ bariyo/uporo – chakula kilicholala mpaka asubuhi.
- Ukoko – mabaki/ masazi ya chakula yanayoganda kwenye chombo kilichopikia chakula hicho.
- Staftahi – kifunguakinywa
- Kisabeho – chakula cha asubuhi.
- Kishuka/ chamcha – maakuli ya adhuhuri
- Kilalio/chajio – chakula cha jioni
- Masizi – unga mweusi wa makaa au moshi ambao aghalabu hupatikana kwenye sufuria au chungu cha kupikia.
- Utandu – masalio yaliyomwagika chakula kinapopikwa.
- Viungo – vitu vinavyotia chakula ladha au harufu nzuri k.m. chumvi, kitunguu, iliki, karafuu, masala, bizari, tui,
- Mlale – Utandabui mweusi utokanao na moshi jikoni.
- Chungu – chombo cha kupikia.
- Kata – chombo cha kuchotea maji mtungini.
- Mbuzi – chombo cha kukunia nazi.
- Susu – chombo cha kuwekea sahani au chungu.
- Mwiko – kifaa cha kupakulia, kusongea au kukorogea chakula.
- Buli/birika – chombo cha kutilia chai au kinywaji kingine.
- Kinu – chombo cha kusagia nafaka, viungo n.k.
- Kikaango – chombo kinachotumiwa kukaangia vyakula k.v. chapati au mayai.
- Kifumbu/kunguto,kichujio – chombo cha miyaa cha kuchujia nazi.
- Kikamulio – kifaa cha kukamulia matunda ili kuyatoa maji yake.
- Deste – Sahani kubwa ya kuwekea halua.
- Degi – sufuria kubwa ya kupikia chakula kingi.
- Sinia – sahani kubwa ya mviringo itengenezwayo kwa madini – hutumika kupakulia chakula.
- Chano/fua – sinia kubwa ya ubao ya kupakulia chakula.
- Tanuri – jiko la kuokea mikate.
- Jokofu/friji/ jirafu – chombo mfano wa kabati chenye mtambo wa kuleta baridi na kuhifadhi aghaabu vyakula.
- Kihoro – sahani ya mti.
Vitendo jikoni
- Kukoka moto – Asha moto.
- Kupuliza moto – Kusababisha moto uwake kwa nguvu zaidi.
- Kuzima moto – kupoesha moto.
- Kuteleka/ kuinjika – kuweka chungu juu ya jiko.
- Kuepua – kuondoa chungu juu ya jiko.
- Kutokosa – kuchemka Kutokota – chemka kwa nguvu.
- Kupepeta – rusharusha nafaka katika ungo kuondoa makapi