Maswali kadirifu

A. Kamilisha maswali kuhusu makao ya viumbe

 

1. Kasuku huishi kwenye _____.

2. Nyuni huishi kwenye sasa au _____.

3. Ng'ombe huishi zizi,_____ au _____.

4. Mtawala hukaa kwenye _____.

5. Kina mama hujifungulia kwenye _____.

6. Konokono hukaa kwenye _____.

7. Buibui hukaa kwenye _____.

8. Mchwa hukaa kwenye _____, _____, _____, au _____.

9. Makao makuu ya malikia ni _____.

10. Makao ya rais ni _____.

11. Kipepeo huishi kwenye _____.

12. Koo huotamia kwenye _____.

13. Wachawi hukutainia kwenye ____.

14.  Kambi ya wenye ukoma ni _____.

15. Fuko huishi kwenye ____.

 

B. Hapa ni wapi?

  • maganjo     vifusi
  • majilisi        matule
  • pambajio     kilinge
  • shambiro     mkahawa
  • shule           bwalo
  • leba             masjala
  • bohari          unyago
  • jando            bunta
  • ulingo          mimbari
  • stendi          angatua
  • handaki       sebule
  • malishoni     bweni
  • dungu          hekalu
  • mava           bunge
  • ikulu           bangwa

 

C. Kamilisha nomino za makundi.

1. mshumbi wa _____.
2. mzengwe wa _____.
3. kipeto cha _____.
4. mkuo wa _____.
5. chano cha _____.
6. kidani cha _____.
7. kipini cha _____.
8. ramramu ya _____.
9. tume ya _____.
10. tano ya _____.

 

D. Chagua majibu sahihi kati ya yale yalyo mabanoni.

1. Yungwa ni aina ya _____. (matunda,viazi)

2. kula mi mlo, kuja _____. (mjo, waja)

3. Kiungo kinachotakasa damu mwilini huitwa figo _____. (buki, kia)

4. Viazi vitamu huitwa  _____. (sena,msena).

5. Kuwaza na kuwazua ni kupiga _____. (hatua, alinacha)

6. Mahali ardhini wanamojificha wanajeshi kwa nia ya kuwavizia maadui huitwa _____. (ngome, handaki).

7. Genge ni la wezi, pia genge ni la _____. (kazi, kioski, wafanyakazi)

8. Sehemu ya juu kwenye mlima wa volkano huitwa _____. (korongo, nguu)

9. Kaukau _____. (Hukombwa, hugegedwa).

10. Ng'ombe huroroma, simba _____. ( huguruma, hunguruma).