Nomino za makundi |
---|
Maswali kadirifu |
Vipeto, hombo, madonge, matopa, majora, minofu, jumuia, mashunge, matuta, tita.
1. Mama alinunua ______ la samani.
2. Wasasi waligawana ____ ya nyama.
3. Msomi huyo alikuwa na _____ ya vitabu.
4. Tarishi alibeba _____ vya barua.
5. Shambani kulionekana ____ ya udongo.
6. Nilimwona mjakazi aliyebeba ____ la kuni.
7. Washonaji walinunua ____ ya vitambaa.
8. Jitu hilo lilibugia ____ ya sima.
9. Tuliyakata ____ ya mpunga.
10. Viongozi wa _____ ya madola walikutana jijini.
1. Mnamo msimu wa kiangazi mawingu ya __________ yalionekana angani.
2. Tuliliona ______ la ng’ombe huko malishoni.
3. Wakati wa usiku ______ za nyota zilionekana mbinguni.
4. Mrembo huyo alikuwa na ______ ya vipuli ndeweni.
5. ______ la mawaziri lilikutania huko ikulu.
6. Wezi hao walitiwa mbaroni wakiwa na ______ vya nguo vya wenyewe.
7. Mchuuzi huyo alibeba ________ ya mayai.
8. Seremala yule alinitengenezea _______ ya fanicha ya kifahari.
9. _______ hilo la takataka lilinuka fee!
10. Akina mama hao walitunukiwa ____ ya leso.
11. Kijana huyo alijuta aliporushia _______ wa nyuki mawe.
12. Wachapishaji walikuwa na ________ ya karatasi.
13. Barabarani kulionekana ________ wa magari.
14. __________ cha wachawi kulifumaniwa huko mwituni kikipanga njama.
15. ________ la waandishi lilikutana kurati•bu mikakati ya uandishi.
16. Mwanamke huyo alikuwa na _________ la nywele la kupendeza.
17. Tuliyameza __________ ya maji ili kukatia kiu.
18. _________ cha askari kilifika kuzima ghasia za wagomaji.
19. Muthoni ameteuliwa kwa ____ ya shule.
20. Shangazi Nyokabi atanunua ________ ya sahani.