Nomino za makundi |
---|
Maswali kadirifu |
- Nomino za makundi hutumika kuonyeshea mkusanyiko wa nomino au nauni nyingi.
- Nomino za makundi zinaweza kuwa za viumbe k.v. watu au vitu k.v. magari.
Kaumu (i-zi): Umati wa watu fulani.
Mfano katika sentensi: Niliona kaumu ya wafuasi katika mji.
b) Halaiki ya watu
c) Umati wa watu
d) Hadhara ya watu
e) Sisisi ya watu
f) Sufufu ya watu
g) Msafara wa watu
Mkururo (u-i: mfuatano wa vitu au watu mmoja baada ya mwingine.
Mlolongo (u-i): mfuatano wa vitu au watu mmoja baada ya mwingine.
Funda; Ujazo wa chakula au kinywaji kwenye kinywa na kuvimbisha mashavu. Katika sentensi; Piga funda la maji.
Chemchemi
- Chemchemi pia inaitwa bubujiko.
- Chemchemi ni mahali maji yanapopenyea kutoka arthini.
Jozi (i-zi); vitu viwili vilivyo pamoja na vinavyofanana.
- Pia gora(i-zi), kwa mfano gora ya leso.
- Vipande viwili vya kitambaa kama vile kanga, kitenge vinavyofanana au aina moja.
Bunda; Fungu la vitu kama karatasi au nguo vilivyofungwa pamoja.
Shungi; nywele ndefu au manyoya yaliyotokeza mbele ya kichwa cha mtu au ndege.
Seti; Fungu la vifaa au vitu vya aina moja vinavyohusiana katika kukamilisha shughuli fulani.
Halmashauri ni kikundi cha watu maalumu walioteuliwa au kuchaguliwa kuelekeza jambo. Pia kikundi hiki kinaweza kurejelewa kama, bodi.
Baraza (i-zi); kikundi cha watu walioteuliwa au kuchaguliwa na kupewa madaraka maalum.
Mnofu (u-i); nyama isiyo na mifupa au mwiba.
Tanuri (li-ya); jiko lililojengwa ambalo linatumika kuchomea vitu k.v. chokaa, vyombo vya udongo au mikate.
Donge (li-ya); Kitu cha mviringo kilichoshikamana. Tazama pia neno bonge, tufe.
Tone (li-ya); sehemu ndogo ya kitu kiowevu kinachondondoka. Matone ya mvua, maji, dawa, kemikali, na kadhalika.
Kifurushi (ki-vi); vitu vilivyofungwa pamoja kwa karatasi na gundi, nguo au kamba.
Karne (i-zi); Muda wa miaka mia moja.
Korija (i-zi); vitu vya aina moja, kama vile miti, shanga, au nguo vikiwa ishirini ishirini pamoja.
Kundi (li-ya); mkusanyiko wa vitu, watu au wanyama.
Misitu (u-i); Mahali penye miti mingi, mikubwa na midogo, vichaka na hata nyasi.
Kanzi; chakula kilichpikwa pamoja kwa kuchanganywa mchele, pojo, bizari, nyama, pilipili, na samli.
Kichaka (ki-vi); mahali penye miti mifupimifupi iliyoshonana na nyasi, miiba na kadhalika. Pia huitwa kituka
Robota (li-ya); mtumba mkubwa wa bidhaa uliofungwa pamoja kama vile nguo, pamba ili kusafirishwa.
Korija (i-zi); vitu vya aina moja, vikiwa kwa idadi ya ishirini.
Jora (li-ya); bunda la kitambaa lenye urefu wa mita 27.
Mfano, mtumba wa majora.
Kopo (li-ya);
1. Chombo cha chuma au bati, kinachotumiwa kuchotea kitu au kutilia kitu.
2. Bomba la kuteremshia maji kutoka kwenye dari la nyumba.
3. Hutiwa pembeni mwa bati ili kukingia maji ya mvua.
Darzeni/dazeni (i-zi); Jumla ya vitu kumi na viwili.
Kigaro (ki-vi); mkusanyiko wa watu wenye nia ya kumsema mtu vibaya au kumpangia jambo la kumdhuru, au kumdharau na kumfedhehi.
Jopo (li-ya); Kikundi cha watu waliokusanyika pamoja ili kufanya kazi maalum. Pia paneli.
Baraza (i-zi); kikundi ya watu waliochaguliwa na kupewa madaraka maalum ili kutekeleza majukumu fulani.
Genge (li-ya); kundi la watu wanaofanya kazi pamoja.
Pakacha (li-ya) - kikapu kilichosukwa kwa makuti ya mnazi.
Kichala (ki-vi); Kitawi cha matunda yaliyo mengi pamoja. Kichala pia huitwa kichaa.
Kifungu (ki-vi); kipimo cha vitu vilivyotengwa pamoja. Kama vile matunda na viazi.
Kikonyo (ki-vi); - kishina cha tunda au ua ambacho hujishikilia kwenye tawi la mti.
Maana ya bumba;
1. Mfuko mdogo, wa majani ya chai, wa tumbako.
2. Fungu la vitu au wadudu kama vile kikundi cha nyuki waliosongamana na kushikana sana.
Mkungu (i-zi); sehemu ya mgomba yenye ndizi.
Chano (ki-vi); sinia kubwa la ubao la kupakulia chakula.
Kikoa (ki-vi); umoja au ushirika wa watu wanaofanya mambo yao au kazi zao kwa zamu.
Kipeto;
1. Kifurushi kilichfungwa vizuri ili vitu vilivyo ndani yake visisambaratike.
2. Gunia la vitu.
Safu (i-zi); mstari aghalau wa watu waliojipanga mmoja nyuma ya mwingine.
Kilenge (ki-vi); mahali pa uganga.
Kikosi (ki-vi); mkusanyiko wa askari zaidi ya elfu moja, huwa chini ya meja.