Maswali kadirifu

A.  Tumia neno jingine lenye maana sawa na lililoandikwa kwa wino uliokolea

Hayawani, chudi, njozi, matatizo, ugani, wahaka, nilihama, wanalandana, zawadi, kurunzi, ngeu, aushini, soka.

 

1. Mtoto huyu alikuwa na bidii kupita kiasi.
2. Askari alitumia tochi kumulikia.
3. Usiku huo nilipata ndoto ya ajabu.
4. Maishani mwangu sijalaza damu.
5. Masaibu yaliponizidia, niligura mjini.
6. Wanafunzi walicheza kandanda huku uwanjani.
7. Niliingiwa na wasiwasi m wenzangu alipokosa kufika.
8. Huko msituni, tulimwona mnyama wa ajabu.
9. Ndugu hao wanafanana kama Kurwa na Doto.
10. Aliposhinda, alipata tuzo.

 

B. Andika visawe viwili vya kila neno lifuatalo:

a) mpagazi       b) msichana         c) adabu           d) duni

e) makao          f) huzuni              g) afya              h) aibu

i) moyo            j) mwizi               k) busara           l) kasoro

m) kimatu        n) cheo                 p) shamba        q) umri

r) bingwa          s) dalili                t) dhiki             u) fikiri

 

C. Andika visawe zaidi ya moja kwa kila neno lifuatalo:

a) konde   b) chemchemi    c) nderemo       d) ngedere  e) ibada  

f) daawa        g) ijara         h) umahiri       i) masaibu   j) gombo

k) ngamizi    l) shauku     m) ndwele        n) kibali      p) panka       

q) kambarau  r) siha         s) kuzimu          t) nikaha     u) pululu

v) mlozi         w) mkwasi        x) mwele     y) mwangazi

 

D. Teau visawe vya maneno yanayofuata

  • redio -
  • kompyuta -
  • shahari -
  • ritifaa -
  • kaptura -
  • moyo -
  • mwangwi -
  • zagaa -
  • mgunda -
  • maisha -
  • kipindupindu -
  • maradhi -
  • maringo -
  • siahi -
  • pure -
  • seuze -
  • siku -
  • shaghalabaghala -
  • silika -
  • masika -
  • afya -
  • ashekali -
  • banati -
  • landa -
  • mia